LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 8, 2012

Tume ya Katiba yandelea na Kazi Mkoa wa Pwani.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwaseni wilayani Rufiji mkoani Pwani katika mkutano wa kukusanya maoni yao kuhusu katiba Mpya. Wengine ni wajumbe wa Tume hiyo Bw. Ally Saleh, Bi. Fatma Said Ally na Bi. Al Shaymaa.
Wananchi wa kijiji cha Mloka, Kata ya Mwaseni wilayani Rufiji, mkoani Pwani wakimsikiliza Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu katika mkutano wa kukusanya maoni yao kuhusu Katiba Mpya.

Timu ya tume ya kukusanya na kuratibu maoni juu ya mabadiliko ya Katiba imeweka kambi katika wilaya ya Rufiji ambapo wanatembelea vijiji mbalimbali kukusanya maoni ya wananchi juu ya mabadiliko ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Zoezi la ukusanyaji limeonekana kuanza kwa kasi na mafanikio makubwa kwani hakuna dosari za kimsingi ambazo zimeripotiwa mpaka hivi sasa juu ya utaratibu ama utendaji wenye mashaka wa tume hii iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho kikwete.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages