Chama Cha Mapinduzi, kupitia Idara ya oganaizesheni, chini ya Katibu wa NEC organaizesheni Ndugu. Asha Abdallah Juma, kinaendesha mafunzo kwa makatibu wa wilaya yanayolenga kuboresha utendaji wa Chama katika ngazi ya wilaya.
Mafunzo hayo ambayo yalianza rasmi Jumatatu tarehe 4th June 2012, yalifunguliwa na Katibu wa Organaizesheni Bi Asha Abdallah Juma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,Ndg Wilson Mukama. Ambapo Mgeni mualikwa katika semina hiyo alikuwa ni Mzee Kingunge.
Aidha, Mada na Taarifa mbalimbali ziliwasilishwa kwa makatibu hao wa wilaya ambazo zilibeba maudhui ya kuimarisha na kuboresha dhana mzima ya utendaji ndani ya Chama kulingana na Mabadiliko ama mageuzi ambayo Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kiliyapitisha na kukubaliana.
Semina hiyo inaendelea ambapo Mada mbalimbali zimekuwa zikiendelea kuwasilishwa na wafafanuzi mbalimbali. Semina hiyo inategemewa kumaliza tarehe 08th June 2012.
Wenezi wa ngazi za chini waamke wamelala mno...
ReplyDelete