LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 6, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGANA NA BALOZI WA CANADA ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Balozi wa Canada nchini Mhe. Robert J. Orr


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Asubuhi ya leo, tarehe  06 Juni 2012, alimkaribisha Balozi wa Canada nchini Tanzania, ambaye amemaliza muda wake Mhe. Robert J. Orr. katika Ofisi yake iiliyopo maeneo ya Ikulu Jijini Dar es salaam. 

Balozi huyo alimtembelea Makamu wa Rais kwa lengo la kufanya nae mazungumzo ya kuagana, kwa kuwa muda wa Balozi huyo kuwepo nchini umekwisha. Akizungumza na Makamu wa Rais, Balozi Orr aliendelea kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi yake ya Canada utaendelea kuimarika licha ya kuwa yeye kuondoka Tanzania.

Balozi Orr anategemea kuondoka nchini mwanzoni mwa wiki ijayo.


Makamu wa Rais. Dkt Mohammed Gharib Bilal akiagana na Balozi Robert. J Orr.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages