Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Wilson Mukama, amehudhuria Mkutano wa Vyama rafiki vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika uliofanyika tarehe 8th june 2012 katika hoteli ya Rainbow Tower Hotel, jijini Harare, Zimbabwe.
Mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Viongozi wa Vyama hivyo rafiki, ambao ni Makatibu Wakuu wa sasa wa Vyama vilivyopigania Ukombozi Kusini mwa Afrika ambavyo ni ANC, CCM, FRELIMO, MPLA, SWAPO na ZANU-PF. Makatibu Wakuu hao ni komredi Gwede Mantashe, Wilson Mukama, Filipe Paunde, Juliao Mateus Paulo "Dino Matrosse" na Didymus Mutasa, ambapo kwa Chama Cha SWAPO kiliwakilishwa na Makamu Katibu Mkuu Komredi Nangolo Mbumba.
Mkutano huo, ambao ulifunguliwa na Rais wa Zimbabwe ambae pia ni Katibu Mkuu wa ZANU-PF, Komredi R.G MUGABE, ulitanguliwa na Mikutano ya Wazee, Wanawake na Vijana wa Vyama hivyo, iliyofanyika tarehe 07 June 2012.
Aidha, Ajenda za mkutano huo zilikuwa ni
(i) Kuanzisha Chuo Cha Pamoja Cha Vyama Hivyo.
(ii) Ripoti juu ya hali za nchi.
(iii) Mikakati ya Ushirikiano katika Chaguzi za Chama.
(iv) Kupitia makubaliano ya Mkutano wa wazee, wanawake pamoja na vijana.
(v) Mipango na Ratiba za Mikutano mwaka 2012-2013.
Pamoja na mambo mengine umefanya maazimio ya kujenga Chuo cha Siasa katika eneo la Ihemi, Iringa Nchini Tanzania. Ambapo Chama Cha Mapinduzi kilipewa jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa taarifa muhimu za ujenzi ikiwemo ramani na jografia ya eneo husika.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anatarajia kurudi Nchini, mwanzoni mwa wiki ijayo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha ZANU-PF ambae pia ni Rais wa Zimbabwe. Comrade Robert Mugabe akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano huo. |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇