Mwenyekiti wa CCM, Rais Jaklaya Kikwete akizindua Blogu hii na Tovuti Rasmi vyote vya Chama, hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Wanaomwelekeza ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Suleyman Mwenda ambaye ni Mkuu wa masuala ya Teknolojia Mawsiliano, Idaya ya Mawasiliano na Umma Makao Makuu ya CCM. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. Tovuti ya CCM ni www.ccm.or.tz kuiona BONYEZA HAPA
Nape akitoa maelezo kuhusu Tovuti na Blogu hizo zinavyoendeshwa na faida zake kwa CCM
Nape akiendelea kutoa maelezo
Nape akimshauri jambo Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Amani Abeid Karume.
Rais Kikwete akiwa na mwenyeji wake katika uzinduzi huo Nape Nnauye wakati akiwasili.
Nape akitoa hotuba fupi kuhusu Tovuti na Blogu hii
Katibu wa CCM Wilson Mukama akimkaribisha Rais Kikwete kuzindua Blogu hii na Tovuti (Website Rasmi ) ya Chama.
Ikafuatia burudani ya hali ya juu iliyoporomoshwa na bendi ya Super Melody ya CCM. huku Nape akionyesha umahiri wake wa kucharaza gita na bendi hiyo.
Watu wananogewe na umahiri wake; Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akimpongeza Nape kwa umahiri huo wa kucharaza gita.
Watu wakamtuza Nape
Mmoja wao ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere kama anavyoonekana akimtuza
Waalikkwa wakaserebuka muziki mpaka hamu yao ilipokwisha
Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akisindikizwa na viongozi kuondoka shughulini
Wakati anaondoka Mjumbe wa NEC Mzee Mtandika akionyesha umahiri mbele yake wa kusakata muziki wa enzi hizo.
"HUYU ASIJE AKATUWEKA KWENYE BLOGU YA CHAMA" wakasemezana wakifurahi Makongoro Nyerere na Waziri Stephen Wasira
Kuserebuka ukaendelea
Viwanja vya Makao makuu ya CCM Dodoma pakawa hapahoshi.
Mwanzoooni kabisa maandalizi yalikuwa hivi. (Picha zote na Bashir Nkoromo)
Your Ad Spot
May 14, 2012
Home
Unlabelled
JK AZINDUA BLOGU NA TOVUTI RASMI YA CHAMA
JK AZINDUA BLOGU NA TOVUTI RASMI YA CHAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot


















No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇