LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 14, 2021

CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU NYERERE KIBAHA NDIPO FIKRA ZA MWALIMU NYERERE ZITATEKELEZWA KWA VITENDO

 Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa  Mratibu wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) Emmanuela Kaganda yeye na ujumbe wake walipotembelea chuo hicho, Kibaha mkoa wa Pwani, jana.


Kibaha, Pwani

Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah amesema katika Chuo Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) ndipo mahala rasmi ambapo sasa zile fikra zake za kulikomboa Bara la Afrika zitatekelezwa kwa vitendo kwa sababu watapatikana viongozi ambao watakuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa kuwa  mafunzo watakayopata hapo yataakisi na yataelekeza Itikadi na falsafa za Mwalimu Nyerere.


Mama Anna Abdallah alisema hayo, jana wakati yeye na  Wajumbe wa Baraza hilo  walipo walitembelea  Chuo hicho kilichopo eneo la Kibaha katika mkoa wa Pwani kwa ajili ya kujionea  ujenzi wa kisasa uliofanyika na kushuhudia mambo mbalimbali kabla ya kuanza kwa masomo ya Uongozi katika chuo hicho..


"Sote tumeshuhudia hata baadhi ya watoto wa Viongozi ambao wamelelewana kuishi maisha yao yote ndani ya CCM, kuwa ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kusema mabaya kuhusu nchi ya Tanzania na kuharibu taswira ya nchi hii, hayo yataondoka kwa watu kuja kujifunza uzalendo katika chuo hiki , kwa sababu kiongozi mzuri anajengwa na kufundishwa Uzalendo wa Taifa lake.


Jina la Mwalimu Julius Nyerere limetumika katika maeneo mengi, lakini katika Chuo hicho ndipo mahala rasmi ambapo sasa zile fikra zake za kulikomboa Bara la Afrika zitatekelezwa kwa vitendo kwa sababu watapatikana viongozi ambao watakuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa kuwa  mafunzo watakayopata hapo yataakisi na yataelekeza Itikadi na falsafa za Mwalimu Nyerere", alisema Mama Anna. 


Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Baraza hilo Mama Anna Abdallah aliongozana na Wajumbe wa Baraza ambao ni Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Pandu Omer Kificho, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kepteni Mstaafu John Chiligati,  Charles Singili na Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay.


 Wengine kwenye Msafara huo walikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Bara Rodrick Mpogolo ambaye ndiye  Katibu wa Sekretalieti ya Baraza hilo la Wadhamini wa CCM, Katibu wa NEC - Uchumi na Fedha Zanzibar  Afadhali Afadhali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mwalimu Raymond Mwangwala ambaye pia ni Mjumbe wa NEC.

Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chuo Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School), baada ya kutembelea chuo hicho, jana, Kibaha mkoa wa Pwani, jana.

5 comments:

  1. Tafadhari ninaomba kujua namna ya kujinga na chuo cha siasa na uongozi bora

    ReplyDelete
  2. Ni jambo jema kikubwa nikupata vijana watakao fata misingi na maadili ya uongozi pia nashauri kipaumbele wapewe walimu waliopo makazini naamn hawa ndyo utakuwa msingi mzuri wa uongozi.

    ReplyDelete
  3. Pongezi sana kwa chama chetu kwa kuanzisha shule ya uongozi.
    Ombi langu sisi wengine Ni watumishi kada ya elimu mutuombee kwa waajiri wetu ili watupe ruhusa ya kuja kusoma

    ReplyDelete
  4. Kuna ulazima wa hizi kozi kufundishwa hata katika level ya chini ya elimu I'll kuwaanda viongozi wa baadae mfano kuwe na certificate pamoja na diploma za uongozi ambazo mtu yeyoye akipenda ataenda kusoma

    ReplyDelete
  5. Ninaomba kujua vigezo vya kujiunga na chuo hicho au nipataje taarifa za chuo hicho

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages