• Home
  • About CCM's Official Blog
  • Contact/Mawasiliano

CCM Blog
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • KIJAMII
    • SIASA
    • BIASHARA
    • UCHUMI
    • MICHEZO
    • BURUDANI
    • MAKALA
    • MAGAZETI
  • LATEST HEADLINES👉

    • featured

      POLISI WATOA UFAFANUZI MADAI YA ACT WAZALENDO

    • Elimu

      WIZARA YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA VIONGOZI WA ELIMU NCHINI

    • Afya

      RAIS DK. SAMIA AIIMARISHA MARADUFU MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI, YAWEKEZA MITAMBO YA KISASA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIMAABARA

    • featured

      MAMA ANNA MKAPA, JANETH MAGUFULI WATEMBELEA BANDA LA BUNGE SABASABA

    • Elimu

      PROGRAMU YA SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP DS/AI+ YAZINDULIWA NELSON MANDELA

      

    Jun 27, 2020

    Home featured Sanaa DIAMOND PLATNUMZ ANAVYOLINGANISHWA NA WASANII WENGINE AFRIKA KATIKA MTANDAO WA YOUTUBE

    DIAMOND PLATNUMZ ANAVYOLINGANISHWA NA WASANII WENGINE AFRIKA KATIKA MTANDAO WA YOUTUBE

    Richard Mwaikenda June 27, 2020 ,featured ,Sanaa


    Diamond Platnumz akishangazwa na wazalishaji wake wa muziki nyumbani kwake
    CHANZO CHA PICHA,WCB_WASAFI
    Diamond Platinumz alishangazwa na wazalishaji wake wa muziki wiki iliopita walipoingia katika nyumba yake na keki iliokuwa na nembo ya kuadhimisha hatua muhimu ya nyota huyo wa Tanzania.
    Huku akipigwa picha akivalia nguo , mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 30 aliambiwa na kundi lake kwamba ndiye msanii wa kwanza katika jangwa la sahara kupata views bilioni moja katika chaneli ya Youtube.
    Ruka Instagram ujumbe, 1
    Mwisho wa Instagram ujumbe, 1

    Presentational white space
    Katika kipindi cha miaka 10 iliopita, mwanamuziki huyo alieshinda mataji kadhaa amekuza muziki wa bongo fleva kuwa maarufu - muziki wa kipekee wa Tanzania unaotoa nyimbo za kimapenzi zilizochanganywa na midundo ya kisasa inayotokana na muziki wa jadi wa taarab kutoka pwani ya Afrika.
    Diamond Platinumz ni mwanamuziki alie na bidii na maonyesho yake huvutia mashabiki wengi, kulingana na DJ Edu, ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha runinga cha kila wiki cha muziki wa Afrika cha BBC.
    • Jinsi virusi vya corona vinavyoathiri burudani
    • Diamond ajitetea kuhusu mwanawe Daylan
    Huku akiwa na asilimia 43 ya mashabiki miongoni mwa raia milioni 55 nchini Tanzania wanaoweza kuingia katika mtandao, kupitia simu aina ya smartphones, kuna mashabiki wengi wanaopenda muziki wa bongo fleva walio tayari kusikiliza muziki wake wa mapenzi.
    Wanamuziki wengine kama Harmonize pia nao wamebobea katika YouTube.

    Je Views bilioni moja ni nyingi kiasi gani katika YouTube?

    Ni vigumu kubaini umuhimu hasa wa nambari bilioni moja , ikizingatiwa kwamba Diamond Platinumz ana wafuasi wengi katika mtandao wa Instagram ikilinganishwa na wafuasi wake katika YouTube ambao ni milioni 9.7 ikilinganishwa na milioni 3.7.
    DJ Edu anasema kwamba Instagram ni mtandao wenye ushawishi mkubwa kuhusu mtindo wa maisha na majukwaa mengine kama vile TikTok , ambayo inaruhusu sekunde 30 za hakimiliki ya utumizi wa bure wa nyimbo - ni njia nzuri ya kuwanasa wafuasi vijana.
    ''Nyimbo nyengine zinasambaa sana kupitia TikTok , kama wimbo mpya wa Diamond Platinumz kwa jina Quarantine'', anasema
    Ruka YouTube ujumbe, 1
    Maelezo ya video,Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

    Mwisho wa YouTube ujumbe, 1

    Presentational white space
    ''Hii inaweza kuwavutia wafuasi katika mtandao wa YouTube , ambapo fedha zinaweza kupatikana kupitia matangazo.
    Muhumu zaidi kwa wanamuziki barani Afrika , katika muongo mmoja uliopita YouTube imewaruhusu kuingia moja kwa moja kupata mashabiki , badala ya kutegemea stesheni za runinga.

    Je analinganishwaje na nyota wengine wa Afrika?

    Diamond Platnumz bado yuko nyuma ya wanamuziki wengine wa eneo la Afrika ya kaskazini ambao wana mashabiki wengi katika eneo la mashariki ya kati.
    Na vilevile kuna wasanii wanaoishi Afrika kama mwanamuziki aliyezaliwa Mali Aya Nakamura , ambaye anampiku mwanamuziki huyo wa Tanzania kwa Views zaidi ya bilioni 1.7 katika YouTube

    Aya Nakamura katika onesho lake la muziko Ufaransa 2019
    CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

    Maelezo ya picha,
    Aya Nakamura alijipatia umaarufu wake kupitia wimbo wake Djadja
    Msichana huyo alielekea Ufaransa wakati alipokuwa msichana mdogo na kujipatia umaruufu mkubwa kupitia wimbo wake wa 2018 Djadja.
    Na Akon mwanamuziki wa Senegal aliyebadilika na kuwa Rappa wa Marekani anawashinda wote kwa Views bilioni 3.5.
    Katika Afrika ya jangwa la sahara, washindani wa Diamond Platinumz katika mtandao wa You Tube ni wasanii wa Nigeria.
    • P Square - 810 million
    • Davido - 618 million
    • Flavour - 617 million
    • Tekno - 574 million
    • Burna Boy - 507 million
    • StarBoy TV (AKA Wizkid) - 480 million
    Takwimu za wasanii Davido na Burna Boy ndio zinazovutia zaidi ikizingatiwa kwamba walifungua chaneli zao za YouTube mwaka 2018.
    Diamond amekuwa katika ukumbi huo tangu 2011.

    Na kampuni ya kurekodi muziki ya Wizkid , StarboyTV - unapoongezea takwimu kwa chaneli zake nyengine ana takriban Views Milioni 802.
    Nyota wengine hupendelea kuwa na chaneli zao wenyewe ili kukuza nyimbo zao na kuondoa urasimu kwa kuwa kampuni nyingi za muziki huchukua muda mrefu kutoa nyimbo mpya.
    Majina mengine maarufu ni Magic System ya Wizkid .
    Nyota wengi hupendelea kumiliki chaneli zao wao wenyewe ili kukuza nyimbo zao na kupunguza urasimu kwa kuwa kampuni hizo za kurekodi muziki huchukua muda mrefu kutoa nyimbo mpya. Kampuni nyengine maarufu ni Magic System ya Ivory Coast ilio na zaidi ya views milioni 477.
    Kundi hilo ni maarufu hususan katika maeneo ya magharibi mwa Afrika ambapo wenyeji huzungumza Kifaransa.
    Ufuasi huu unatokana na wimbo wao Gaou- ni wimbo mmoja ambao umefanikiwa kuliunganisha bara zima , kulingana na DJ Edu.
    Huku takwimu za chini za You Tube miongoni mwa wasanii wa Afrika Kusini zikiponza umaarufu wao, wana uwezo wa kujipatia fedha kupitia kampuni zao wenyewe za muziki , anasema Dj Edu. Na kama unavyojua YouTube sio chaneli ya pekee ilio na huduma ya streaming.
    Wizkid alifanya kazi na rapa wa Canada Drake mwaka 2016 - ambapo wimbo wao wa One dance - ulioonyeshwa zaidi ya bilioni 1,8, lakini hakutolewa rasmi katika mtandao wa YouTube.

    Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

    • Manu Dibango in 2014

      Manu Dibango: The saxophone legend who inspired a disco groove

      28 Machi 2020
    • John Nzenze and Daudi Kabaka

      John Nzenze: The founder of 'Africa's best band'

      13 Juni 2020
    • Members of the Albatross Muf Rockers playing in Zambia

      Letter from Africa: In search of Zambia's glam rockers

      23 Disemba 2019
    Tags featured# Sanaa#
    Share This
    Author Image

    About Richard Mwaikenda

  • MAANDALIZI TAMASHA LA WANYAKYUSA YAPAMBA MOTO DAR ES SALAAM

  • TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 60 YA KIDIPLOMASIA NA CHINA, 'AMAZING TANZANIA' YAZINDULIWA RASMI JIJINI BEIJING, CHINA

  • NAIBU WAZIRI 'MWANA FA' APAGAWISHA MKUTANO WA CHONGOLO TANGA

  • By Blog CCM Blog Richard Mwaikenda - June 27, 2020
    Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
    Tags featured, Sanaa
    Newer Post Older Post Home
    Subscribe to: Post Comments (Atom)
    • blogger
    • disqus
    • facebook

    No comments:

    Post a Comment

    MAONI (COMMENTS)👇

    Post Top Ad


    ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI YA 2025/30

    ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI YA 2025/30

    KAULIMBIU YA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

    KAULIMBIU YA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

    WALIOTEULIWA NA CCM KUGOMBEA URAIS, MAKAMU UCHAGUZI MKUU 2025

    WALIOTEULIWA NA CCM KUGOMBEA URAIS, MAKAMU UCHAGUZI MKUU 2025
    Mgombea Urais, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia

    Mgombea Mwenza Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi

    Mgombea Urais wa Zanzibar, Rais Dk. Mwinyi

    Chagua Lugha/Translate Language👇





    Tafuta (Search) hapa👇

    CCM Blog. Powered by Blogger.

    Pages

    • Home


    Idadi ya wanaosoma CCM Blog

    6618758

    Tuma Ujumbe hapa

    Name

    Email *

    Message *

    This Blog Designed and Developed By Bashir Nkoromo | SoraTemplates | Property of Chama Cha Mapinduzi