Apr 20, 2020

UJUMBE WA AFRIKA KUSINI WAWASILI LESOTHO

  Ujumbe wa Afrika Kusini uliwasili leo nchini Lesotho baada ya waziri mkuu wa taifa hilo dogo kuliamuru jeshi kuingia mitaani kabla ya kuliondoa tena.
Ujumbe ukiongozwa na waziri wa zamani wa nishati wa Afrika Kusini Jeff Radebe ulikutana na Waziri Mkuu Thomas Thabane na kisha wanachama wa upinzani na makundi ya kiraia. Afrika Kusini inaizingira Lesotho, na mshirika wake mkubwa kibiashara.

Msemaji wa serikali Thesele Maseribane amesema Afrika Kusini ni jirani yao kwa hiyo wana wasiwasi na kinachoendelea nchini humo.

Siku moja kabla, magari ya kivita yalipita katika mji mkuu Maseru baada ya Thabane kutangaza kuwa ameliamuru jeshi kupambana na watu wenye nia mbaya.

Bila tangazo lolote rasmi, jeshi likajiondoa saa kadhaa baadaye.

Thabane anakabiliwa na ongezeko la miito ya kumtaka ajiuzulu kutoka kwa wapinzani ndani ya chama chake tawala na makundi ya upinzani kuhusiana na madai ya kuhusika na mauaji ya mkewe mwaka wa 2017

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages