Mar 13, 2020

VIRUSI VYA CORONA VYATUA NCHINI KENYA

  Wizara ya Afya nchini Kenya  imeripoti kisa cha kwanza cha virusi vya ugonjwa wa corana . 

Kulingana na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, mgonjwa huyo raia wa Kenya alithibitishwa kuwa na virusi hivyo baada ya kurejea nchini  humo kutoka Marekani, Alhamisi, Machi 5. 

Amelazwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH). Waziri ameripoti kuwa, mgonjwa huyo wa kike aliyejipeleka hospitali mwenyewe baada ya kuhisi maumivu anaendelea vizuri na matibabu na kwamba joto lake la mwili limepungua. 

Mikutano yote ya hadhara, kutembelea wafungwa vimepigwa marufuku kwa sasa na wizara imewataka Wakenya wote kuzingatia usafi wakati wowote

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages