Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jaji Semistocles Kaijage akizungumza na
mkutano na wadau wa uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kupeana taarifa juu
ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa Mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani utakaoanza wiki ijayo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), amesema kitendo cha baadhi wananchi kushindwa kukumbuka majina yao, kinasababisha ucheleweshwaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura.
Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa Wadau wa Uchaguzi, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alipokuwa akitaja baadhi ya changamoto zinazolikabili zoezi hilo.
"Wapiga Kura kushindwa kukumbuka majina yao wanapokwenda kituoni kwa ajili ya kurekebisha taarifa zao na hivyo kuchukua muda mrefu katafuta majina yao kwa usahihi," alisema Jaji mstaafu Kaijage.
Alitaja Changamoto nyingine kuwa ni
kuwepo kwa idadi kubwa ya wananchi waliopoteza kadi zao za kupigia kura ama
kadi zao kuharibika. Nitoe rai kwenu kuwakumbusha wapiga kura
kuhakikisha wanatunza kadi zao hadi siku ya uchaguzi na hata baada ya hapo.
Katika maeneo mengi
kumekuwepo na hali ya watu kujitokeza kwa wingi siku za mwishoni ili kuboresha
taarifa zao au kujiandikisha na hivyo
kusababisha misururu mirefu kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura. Jambo
hili linaweza kuepukika kama wananchi
watajitokeza mapema pindi zoezi linapoanza.
Jambo lingine ni wananchi
wengi katika baadhi ya maeneo kushindwa kutofautisha Daftari
la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa
ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais
na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania
Bara. Tume kupitia Elimu ya Mpiga Kura inaendelea na juhudi za kutoa ufafanuzi
juu ya utofauti wa Chaguzi hizi na mamlaka
zake za Usimamizi.
Changamoto
nyingine ni zoezi hili kufanyika katika kipindi cha mvua kwenye baadhi ya maeneo na hivyo kuathiriwa na
miundombinu ya barabara. Hata hivyo,
Tume ilijipanga kukabiliana na hali hiyo, na kuweza kufikisha vifaa kwa wakati bila
kuathiri ratiba ya kufanyika kwa uboreshaji. Kwa upande wa vituo vya kujiandikisha vilivyo
katika maeneo ya wazi Tume iliandaa mahema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇