LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 3, 2025

KISESA WAMKUBALI DKT. SAMIA, DKT. NCHIMBI

 MAMIA ya Wananchi  wa Kata ya Mwandoya ndani ya Jimbo la Kisesa,wilayani Meatu wakimsikiliza  Mgombea Mwenza wa Urais wa   Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  wakati akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara leo Septemba 2,2025,wakati akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni mkoani Simiyu.


Katika mkutano huo wa kampeni,Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi alimnadi Mbunge wa Jimbo hilo la Kisesa,Musa Godfrey Mbuga pamoja na diwani wa kata ya Lubiga,Juma Mpina ambaye ni kaka wa mbunge wa zamani wa jimbo laKisesa, Luhaga Mpina

Pamoja na mambo mengine Balozi Dkt.Emmeanuel Nchimbi amekuwa akiinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu,Mgombea mwenza wa Urais,wabunge na madiwani wa Chama hicho.




 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages