LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 29, 2017

ZIARA YA POLEPOLE MKOA WA MOROGORO YAWANG'OA KAMATI YA SIASA KATA YA KIDATU WILAYA YA KILOMBERO

Katibu wa Hakmashauri kuu Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Pole Pole akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Kilombero  katika mkutano wa ndani uliofanyika Julai 28, 2017, katika Kata ya Kidatu akiwa katika ziara ya Kichama mkoani Morogoro.

KIDATU, MOROGORO
Wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya kidatu wamejiuzulu nafasi zao za uongozi kwa pamoja na kuomba radhi wanachama kwa makosa ya kushindwa kutoa uongozi madhubuti.

Akiwa katika ziara ya kichama mkoa wa Morogoro Wilaya ya Kilombero kata ya Kidatu, leo tarehe 28 Julai 2017, Katibu wa Halmashauri kuu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu H.H. Polepole alifanya kikao cha ndani,  alipata fursa ya kuzungumza, kusikiliza  na kutatua changamoto mbalimbali za wanachama.

Katika kikao hicho kilichohusisha Wanachama, Viongozi wa Mashina, Halmashauri kuu za Matawi na Kamati ya siasa ya kata ya Kidatu,       Ndugu Polepole aliambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Katibu wa Chama Cha Mapinduz(CCM) Mkoa wa Morogoro, Katibu wa Chama wilaya, Mkuu wa mkoa wa morogoro na mkuu wa wilaya ya kilombero.

Wakati wa kikao hicho kilichoongozwa na Ndugu Polepole baada ya malalamiko na shutuma nyingi kutoka kwa  wanachama dhidi ya viongozi wa CCM kata ya kidatu ikiwemo kushindwa kusimamia uchaguzi wa matawi, kushindwa kusimamia rasilimali za chama,  usaliti wakati na baada ya uchaguzi mkuu hali iliyopelekea CCM kupoteza kata ya kidatu viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM kata ya kidatu Ndugu Mangungu Alex waliomba kujiuzulu nafasi zao zote za uongozi ndani ya chama,   kuomba radhi wanachama wa CCM na kuahidi kubaki kuwa wanachama waaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Akisisitiza uamuzi huo katika kikao hicho cha ndani Ndugu Polepole alisema  Kama mtumishi wetu namba moja kwenye Chama na Serikali yetu Ndugu John Pombe Joseph Magufuli anajua kuwa cheo ni dhamana, wewe mwingine unapata wapi nguvu ya kutumia cheo kwa faida yako

Akitoa neno la kuhitimisha Ndugu H.H. Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinafanya mageuzi makubwa ya kurejesha chama kwa wanachama, kusimamia rasilimali za chama zitumike kwa manufaa ya chama, kujenga misingi imara ya utoaji haki ndani ya chama pamoja na kuhakikisha katika chaguzi zinazoendela CCM inapata viongozi wenye sifa “Haipaswi wakati wowote kugeuza Chama hiki kuwa chama cha viongozi, Chama hiki tangu awali msingi wa kuanzishwa kwake ni kuwa kiwe chama cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu

Pia Ndugu Polepole amempokea na kuagiza uongozi wa ngazi ya tawi kumpokea na kumpa mafunzo ya Itikadi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) aliyekuwa mgombea udiwani na Mwenyekiti wa ACT kata Kidatu Ndugu Deodatus Makolo ambaye leo amejivua nafasi zake zote za uongozi  katika chama hicho na kujiunga na CCM.

Ndugu H.H. Polepole yupo ziarani Mkoa wa Morogoro, kukagua na kujionea zoezi la uchaguzi wa ndani ya Chama ngazi ya msingi unaoendelea, kipindi hichi ambacho CCM inafanya mageuzi makubwa ya kiuongozi,     kimuundo na kiutendaji. Ziara hii ni muendelezo wa ziara za kichama na vikao vya ndani vyenye lengo la kutoa hamasa,  kuvumisha umuhimu wa Mageuzi ya Chama, kuimarisha Chama na kutatua kero za wanachama.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Julai 28, 2017.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages