Sunday, October 9, 2016

MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO AKAGUA WODI NA KUITISHA KIKAO CHA WAFANYAKAZI HOSPITALI YA SINZAMKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MUHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO
 

Na Nassir BakariMkurugenzi wa Manispaa  ya Ubungo Mh .John L. Kayombo jana alitembelea  na kukagua wodi mbalimbali za wagonjwa  na kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Sinza iliyopo Sinza Palestina.

  
Ziara hiyo  imetokana na hatua ya Mkurugenzi  kutaka kufahamu kero za wafanyakazi na miundo mbinu ya utoaji huduma ya hospitalini hapo.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi alisema amesikitishwa na hali aliyokuta hapo ikiwemo uchakavu wa vitanda ,majengo pamoja na uhaba wa wataalamu wa idara mbalimbali.


“Kwa kweli  nimesikitishwa  na hali niliyokuta, inafika hatua mpaka vitanda vinakuwa chakavu namna hii?” alihoji  Mkurugenzi.


Wakati huo huo Mkurugenzi   ameahidi kufuatilia mapato katika hospitali hiyo kwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki utakaosaidia kukusanya kwa uaminifu na umakini na kuzuia mianya ya wizi wa pesa.

“Nitaajiri watu wa Mifumo ya habari(IT), waje watufunge mitambo ya kielektroniki itakayopunguza mianya ya wizi wa pesa,” alisema Mkurugenzi Kayombo.

Pia alisikiliza kero  zinazowakabali  wafanyakazi wa idara mbalimbhali na kuahidi kuzitatua kwa wakati bila upendeleo wowote.


“Nimesikiliza kero zenu kwa umakini, naahidi kushughulikia  moja baada ya nyingine na nawakaribisha ofisini kwangu muda wowote na kama kuna mfanyakazi ana tatizo lolote asisiste kuniambia," alisema Mkurugenzi Kayombo.

MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO AKIMSALIMIA MGONJWA ALIPOTEMBELEA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA SINZA.

        

MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO KATIKATI AKIWA KWENYE KIKAO NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA SINZA.MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBO AKITOKA NDANI YA CHUMBA CHA MKUTANO HOSPITALI YA SINZA.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.