STDFAA WAMUOMBA WAZIRI NAPE KUHARAKISHA UKAMILISHWAJI WA SERA YA FILAMU HAPA NCHINI

Katibu wa STDFAA, Jafari Makatu akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, 
Kulia ni Mwenyekiti wa STFFAA, Ali Baucha na 
kushoto ni Mdhamini wa Chama hicho,
 Ahmed Olotu.
Na Jacquline Mrisho - MAELEZO
Chama cha Waigizaji wa filam mkoa wa Kinondoni (STDFAA) wamemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhimiza kukamilishwa Sera ya filamu ili ianze kutumika  kuwasaidia wasanii katika mambo mbalimbali hususani ya kisheria.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Chama hicho, Jafari Makatu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na kuzungumzia changamoto zinazowakabili katika tasnia ya filamu nchini.

Makatu amesema kuwa Sheria ya Filamu ni muhimu katika tasnia hiyo hivyo ikiharakishwa itasaidia wadau wa tasnia hiyo kufanya kazi kwa uwazi na usalama wa hali ya juu kwa kuwa watakua wanalindwa na sheria.

“Tunamuomba Waziri wetu Mhe. Nape atuharakishie Sera ya Filamu kwa sababu sheria hiyo itatusaidia kuoanisha mambo mbalimbali ya kisheria kuanzia kwenye uandaaji wa kazi zetu hivyo, kupelekea kufanya kazi kwa  ufanisi na kutoa kazi bora zaidi”. Alisema Makatu../>>SOMA ZAIDI

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.