Friday, December 25, 2015

TAMASHA LA KRISMAS LAFANA DAR

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiinua CD juu kama ishara ya uzinduzi wa album ya kundi la muziki wa kwaya la Wakorinto wa Pili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kwenye Tamasha la Chrismas lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions.
 Katika Tamasha hilo Mheshimiwa Nape alisema kuwa Serikali inatambua juhudi za Wasanii na kuahidi kila msanii atapata stahiki yake anayotakiwa kupata.
 Nape ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu ,alielezea azma ya serikali kuunga mkono juhudi za kampuni ya Msama ya kusaidia watoto yatima.

 Msanii wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya Solomoni Mukubwa akitumbuiza kwa hisia kwenye tamasha la krismass lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es salaam .
 Msanii kutoka Afrika ya kusini Rebecca Malope akiingia ukumbini kwa nyimbo za hisia kwenye tamasha la krismas lililofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.