Saturday, December 5, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE, KWENYE MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA, JIJINI JOHANNESBURG, AHUTUBIA LEO MKUTANO WA MWISHO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati walipokutana kwenye Mkutano wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, wakati wakitembelea Mabanda ya maonesho ya mkutano huo uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. ambapo Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo Dec 5, 2015. Picha na OMR
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing (kushoto)  wakati walipokutana kwenye Mkutano wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, walipokuwa wakitembelea Mabanda ya maonesho ya mkutano huo uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. ambapo Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo Dec 5, 2015. Picha na OMR 
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, na Rais Mstaafu wa awamu ya Tano, Dkt. Jakaya Kikwete, wakiangalia moja ya Ndege ya Kivita ya mfano, wakati walipotembelea Mabanda ya maonesho ya Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo Dec 5, 2015. Picha na OMR
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akiongozana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tano, Dkt. Jakaya Kikwete, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing, wakiangalia moja ya Ndege ya Kivita ya mfano, wakati walipotembelea Mabanda ya maonesho ya Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo Dec 5, 2015. Picha na OMR
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Sudan, Mhe. Bakri Hassan Salih, walipokutana na kwenye mkutano wa mwisho wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini, ambapo Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, pia alihutubia. Picha na OMR 
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipitia 'Document' kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. Picha na OMR
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika ukumbi wa mkutano wakati akijiandaa kuhutubia kwenye Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. Picha na OMR
 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula, kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. Picha na OMR
 
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.