Saturday, November 7, 2015

RAIS DK. MAGUFULI ATINGA GHAFLA WIZARA YA FEDHA JANA

mg1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile alipotembelea ofisi za Wizara ya Fedha.
mg2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipata ufafanuzi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.  Servacius Likwelile wakati wa ziara hiyo.
mg3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na uongozi wa Wizara ya Fedha.
……………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Fedha leo Ijumaa tarehe 6 Novemba, 2015.
Katika ziara hiyo Mhe.Rais alipata fursa ya kutembelea baadhi ya Ofisi za Wizara na baadae  kuzungumza na Viongozi wa Wizara ili kufahamu changamoto ambazo zinaikabili Wizara ya Fedha.
Wakati akimkaribisha Mhe.Rais Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha        Dkt. Servacius Likwelile alimueleza kuwa Wizara ya Fedha inakabiliwa na changamoto kubwa inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani.  Miongoni mwa sababu ni misamaha ya kodi, wafanyabiashara wengi hasa wakubwa kukwepa kodi, makusanyo yasiyoridhisha ya maduhuli na kutokulipwa kwa kodi za majengo. Aidha Dkt. Likwelile alishauri ni bora kuwekwa mifumo mizuri, ikiwemo matumizi ya Tehama na EFDs.
“Pamoja na ziara yangu kuwa ni ya kustukiza nimefurahi sana kukuta Viongozi wote wapo ofisini na wanafanya kazi. Jambo hili limenipa faraja kubwa. Ziara yangu ya kuja hapa nimejifunza na kujua changamoto zipi zinazowakabili”. Alisema Mhe. Rais.
Nimesikia changomoto nyingi na ninaagiza kuwa muhakikishe walipa kodi wakubwa wanalipa kodi na kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kukusanya kodi kikamilifu na si kuwabana wafanya biashara wadogo wadogo.
Mhe.Rais aliwataka Viongozi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii ili kuvuka lengo.
Imetolewa na;
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Ingiahedi C.Mduma
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.