Saturday, November 14, 2015

NAPE AANZA KAZI ZA KULITUMIKIA JIMBO


Mbunge mteule wa Jimbo la Mtama, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini mkataba wa kupata vifaa vya huduma za afya mbele ya Mwambata wa Siasa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Mis Song Rui katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye ameanza kazi ya kuwatumikia wakazi wa jimbo hilo baada ya kusaini mkataba maalum na Ubalozi wa China nchini wa kusaidia vifaa vya huduma ya Afya kwa jimbo la Mtama.

 Ikumbukwe katika kampeni zake Nape aliahidi kulifanya jimbo kuwa la mfano kwa kuboresha huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi Nape alisema " Wakati nimeamua kugombea ubunge nilisema nataka kuwafanyia kazi watu wa Mtama nataka niwe mbunge wa mfano na niliwaahidi nitatatua kero zao mbali mbali na leo nimeanza kwa upande wa huduma za afya ambapo vituo na zahanati kadhaa vitapata vifaa vya matibabu alivitaja baadhi ya vituo ni Mtama, Nyangamala, Chiponda, Namupa, Chiuta,Luo, Nyengedi,Kiwalala na kwengineko."


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.