LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2015

KAMATI KUU YATEUA WATATU USPIKA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC ,CCM Makao Makuu Dodoma akiwa ameshikilia kitabu cha Kanuni za Kamati ya Wabunge Wote wa Chama Cha Mapinduzi.


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika leo Novemba 15, 2015 mjini Dodoma imewateua wana-CCM watatu watakaopigiwa kura na wabunge wote wa CCM ili kumpata mgombea wa CCM katika nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Walioteuliwa kugombea nafasi hiyo na Kamati Kuu iliyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni pamoja na Naibu Spika aliyemaliza muda wake Ndugu JOB NDUGAI, Dkt. TULIA ACKSON na Ndugu ABDULAH MWINYI.



Kwa upande wa Naibu Spika wa Bunge, mchakato wa kuchukua fomu kwa wabunge wa CCM wanaoomba ridhaa kugombea nafasi hiyo utaanza kesho Novemba 16, 2015 na kukamilika Novemba 17, 2015 saa kumi kamili jioni.



Wana-CCM hao watatu watapigiwa kura na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma ilikuchagua jina moja kugombea nafasi hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
 
 Kuhusu nafasi ya Naibu Spika, alisema kulikuwa na kasoro za kutofuata kanuni za chama ambapo hadi jana ni mwanachama mmoja tu ndiye aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu,’ lakini atatakiwa kuchukua fomu upya.
“Ibara ya 57, Kanuni za kamati ya wabunge wote wa CCM toleo la 2010 toleo la nne 2011, mbunge yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Naibu Spika atatakiwa kuchukua fomu kupitia kamati hiyo na atairudisha kisha kamati itakaa kupata jina moja,” alisema Nape.

Kwa mujibu wa maelezo hayo mbunge wa chama hicho anayetaka kugombea Unaibu Spika, atatakiwa kuchukua fomu leo Novemba 16, kwa ada ya Sh 100,000 kisha atairudisha kesho Novemba 17, ndipo kamati itakaa kuchambua na kupitisha jina moja.

 Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo majina matatu yalipitishwa.


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages