LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2015

FILIKUNJOMBE ATEMBELEA WAGONJWA SIKU YA PASAKA



Paroko  wa  kanisa la  anglikana  ludewa  Andrew  Hiluka kushoto akilishwa  chakula na mbnge  wa   jimbo la  Ludewa Deo  Filikunjombe kulia  huku mkuu wa  mkoa  wa Njombe Dr Rehema Nchimbi akimsaidia kushika sahani ya  chakula jana  baada ya  mbunge  huyo na mkuu  wa  mkoa  kuwaandalia chakula wagonjwa  wote  wa  hospitali ya  wilaya ya Ludewa
Mbunge  wa  Ludewa  Filikunjombe  akiongoza  msafara  wa  viongozi  mbali  mbali  akiwemo mkuu  wa  mkoa wa Njombe Dr Nchimbi kutembelea   wagonjwa hospitali ya wilaya ya  Ludewa
Filikunjombe na Rc njombe wakitoa msaada  wa  vitu mbali mbali kama sabuni , mafuta na taulo kwa  wagonjwa  waliyelazwa hospitali ya wilaya ya  Ludewa jana
watoto  wa mbunge Filikunjombe   wakishirikiana na  Rc  njombe  kutoa msaada kwa wagonjwa
Dr  nchimbi na filikunjombe  wakitoa maada wa  chakula na vitu mbali mbali kwa  mgonjwa

mtoto  wa  filikunjmbe akitoa maada wa chakula kwa  mgonjwa
rc njombe  kulia akimlisha chakula  mgonjwa huku  mbunge  filikunjombe  akimsaidia  kushika bakuri
 mbunge Filikunjombe  akimsikiliza mkuu  wa mkoa  wa Njombe Dr nchimbi  wakati akizungumza na  wagonjwa katika hospitali  ya  wilaya ya  Ludewa


 katibu  mwenezi mkoa  wa njombe honoratus  mgaya na mkuu  wa mkoa wa njombe dr  nchimbi wakitoa chakula kwa wagonjwa
 mkuu  wa  wilaya ya  ludewa bw anatory chowa  akitoa maada wa  vitu mbali mbali kwa mgonjwa  hospitali ya ludewa
filikunjombe  akiwa amempakata  mtoto katika  hospitali ya wilaya ya  ludewa
 filikunjombe akitoa msaada  wa  chakula
 mkuu  wa  mkoa  njombe  akila  chakula  na mgonjwa
 filikunjombe  akila  chakula na mgonjwa


 DC Ludewa akila  chakula na mgonjwa 
mwanahabari  wa  TBC Iren Mwakalinga  akila  pasaka na  wagonjwa  hospitali ya  wilaya ya Ludewa






  mbunge  wa Ludewa  Deo  Filikunjombe wa  pili  kulia akishiriki  kula chakula   na  wauguzi pamoja na mmoja kati  ya wanawake waliolazwa  katika  wodi la  wanawake waliojifungua kwenye  hospitali ya  wilaya ya Ludewa  wakati  wa  sikukuu ya pasaka
 mwalimu  DOMINIC HAULE  AKILA  CHAKULA NA  WAGONJWA
 MBUNGE FILIKUNJNOMBE KATIKATI AKILA  CHAKULA NA MUUNGUZI NA MGONJWA  KUSHOTO




 ZIARA  YA  MBUNGE FILIKUNJOMBE NA RC  NJOMBE KWENDA  KULA  CHAKULA NA  WAGONJWA
FILIKUNJOMBE  AKIFURAHI WAKATI WAUGUZI  WA  WAGONJWA  WAKIMSHANGILIA


FILIKUNJOMBE  AKILA  CHAKULA NA MGONJWA 
NA MATUKIODAIMABLOG 
MKUU wa  mkoa  wa Njombe Dr Rehema Nchimbi amempongeza mbunge Ludewa  mkoani Njombe Bw Deo Filikunjombe kwa kutumia sikukuu  ya pasaka  kuwaandalia  chakula watu wenye matatizo  wakiwemo wafungwa wa  gereza la Ludewa  na wagonjwa waliolazwa  katika Hospitali  ya wilaya ya Ludewa  huku akiagiza Halmashauri ya  Ludewa kuanzisha  huduma ya chakula kwa  wagonjwa .

Dr Nchimbi alitoa  pongezi  hizo jana wakati  alipoungana na mbunge  huyo na viongozi  mbali mbali  wa  mkoa na wilaya ya  Ludewa   kushiriki hadla  hiyo ya mbunge  kula chakula pamoja  na wagonjwa  na  kuwapa misaada  mbali  mbali kama ulivyoutaratibu  wake kwa  kila sikukuu kula na wagonjwa na wafungwa .

Alisema  utaratibu  unaotumiwa na  mbunge huyo  ni utaratibu  mzuri  ambao  unapaswa  kuigwa na wabunge  wengine nchini kwa kuyatembelea makundi  mbali mbali ya  kijamii wakati wa  sikukuu ama  siku  nyingine badala ya kusherekea sikukuu kwa  kufanya anasa.

'kweli  ni jambo la kumpongeza   sana  mbunge Filikunjombe  kwa  huu utaratibu  ambao amekuwa akiufanya  binafasi niliposikia mbunge  anakuja  kufanya jambo hili kubwa la  kula  na  wagonjwa  pasaka  niliamua  kufunga  safari na mimi  kuja   kushiriki zoezi hili na  kumtia  moyo  zaidi mbunge kwa   hili si  wabunge  wote ambao  wanakawaida  ya  kutembelea  na  kuwafariji  wagonjwa na  wafungwa  kama  hivi 'alisema mkuu huyo

Hata  hivyo  mkuu  huyo  wa  mkoa  alisema  kuwa  katika   kumuunga mkono  mbunge  Filikunjombe kwa  wazo   hilo  zuri  kwa  upande  wake  anachangia ngunia 5 za  mahindi  ili  kuwaanzishia wagonjwa wanaofika  kujifungua  huduma ya chakula kwa  kipindi chote wawapo  hospitalini hapo kama  njia ya kuepusha wagonjwa  kuwa na  mawazo ya  wapi  watapata  chakula

kwani  alisema  si  wagonjwa   wote  wanaofika   kusubiri muda  wa   kujifungua  hospitalini hapo  wanauwezo wa  kiuchumi hivyo  kuiagiza halmashauri ya  wilaya ya  Ludewa  kuangalia   uwezekano  wa  kuchangisha chakula kwa wananchi  ili  kusaidia  huduma ya chakula kwa   wagonjwa .


Alisema wilaya ya Ludewa na  mkoa wa Njombe kwa  ujumla hauna  shida ya chakula kama   ilivyomikoa  mingine   hivyo uwezekano  wa  kuanzisha utaratibu  wa kutoa  chakula kwa wagonjwa unawezekana .


Akishukuru kwa  msaada  huo  wa  chakula  kwa niaba ya wagonjwa  wengne waliolazwa hospitalini hapo  paroko  wa  kanisa la  anglikana  ludewa  Andrew  Hiluka alisema   kuwa alichokifanya  mbunge huyo  ni  moja kati ya baraka  kubwa  kwake na kuwa baadhi ya wanasiasa  wanapoteza nafasi  zao   kutokana na  kuwa na roho mbaya  na uchoyo kwa  wale   waliowachagua.

Kwani  alisema  Ludewa  imepata   kuwa na wabunge zaidi ya  watano   ila wakati  wa  sikukuu kama   hizo  wabunge  hao  walikuwa wakitoka  nje ya Ludewa ama kujifungia na familia  zao kula sikukuu tofauti na Filikunjombe  ambae  amekuwa  ni  mbunge  wa aina yake kwa  siku ya  sikukuu  kuandaa chakula  cha pamoja na  wagonjwa kwa  kula nao  chakula wodini .

Paroko  Hiluka alitoa   wito  kwa  wananchi  wa   jimbo la  Ludewa  kuendelea kumchangua kwa  miaka mingine  zaidi mbunge Filikunjombe kwani ametambua  mahitaji  sahihi  ya  wana  Ludewa  kwa kusaidia  maendeleo ya   jimbo   hilo pia kuwagusa wote  wenye  matatizo mbali mbali ambao ni nje ya ahadi  zake za ubunge .

Alisema  ni  kipindi  cha  Filikunjombe kasi kubwa ya   maendeleo  imeonekana kwa  kila mwananchi  wa  wilaya   hiyo na nje ya wilaya lakini pia  ni  mbunge  pekee  kusomesha   sekondari watoto  yatima  zaidi ya 700 katika  wilaya   hiyo kwa  kila mwaka  huku wabunge waliopita labda aliyejitiahidi  kusomesha basi haikuzidi watoto 2 kwa miaka yote  mitano .

Nae mbunge Filikunjombe alisema  kuwa utaratibu   huo  wa  kula  chakula na  wagonjwa amekuwa akiufanya kila mwaka toka  alipoingia madarakani  mwaka 2010  na kuwa   iwapo  wananchi  wa jimbo  hili watamchagua ataendelea  kuwaletea maendeleo lakini  pia  kuwasaidia watu wenye matatizo kwani anachoamini na  kuendelea  kuamini  kuwa  wazima na wagonjwa  wote ni  wapiga kura  wake na  kuwa furaha yake  ni  kuona wagonjwa  wanapona ili waweze  kumchagua  tena.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages