Tuesday, January 13, 2015

TANZANIA NA UJERUMANI ZAJADILIANA UHARAMIA DHIDI YA WANYAMAPORI

"Karibu"  ndiyo anavyosema Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi wakati  akimkaribisha  mgeni wake Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya  Ujerumani  katika Umoja wa Mataifa  Balozi  Harld Braun alipofika kwa mazungumzo katika Uwakilishi wa Tanzania siku ya jumatatu.

Wawakilishi hao wawili  walizungumzia masuala mbalimbali yenye maslani kwa  mataifa hayo  mawili,  na moja ya  masuala hayo ni  namna gani  Tanzania na Ujerumani kama   sehemu ya   kundi la nchi ambazo  ziko mstari wa  mbele kupinga na kukemea  uharamia  dhidi ya wanyamapori zitakavyoshirikiana katika majadiliano na  maandalizi ya  rasimu ya  Azimio  kuhusu  uharamia dhidi ya wanyama pori.

Katika  mazungumzo hayo  Balozi Harld Braun  alitambua  juhudi  kubwa zinazofanywa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete  za  kuongoza na kusimamia  mipango  ya serikali  katika  kudhibiti uwindaji haramu wa wanyamapori na hususani Tembo. Ni kwa kutambua Juhudi hizo za Rais Kikwete ndiyo maana Ujerumani  inaiomba  Tanzania  kupitia  Uwakilishi wake wa Kudumu kuwa moja na nchi zitakazo dhamini  Azimio hilo
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.