Monday, January 5, 2015

KINANA AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUICHAGUA CCM KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

  • Mkutano wake waweka historia
  • Atoa salaam za mwaka na kusema Chama kitashughulika na maadili ya viongozi mwaka 2015
  • Asisitiza viongozi kutembelea wananchi na kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa mikutano Tangamano ambapo aliwashukuru wananchi walioichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo Tanga ilichukua nafasi ya pili kwa kupata ushindi wa asilimia 97.
 Wananchi wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyekuja kuwashukuru kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 Baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa kushukuru wananchi kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa January Makamba,Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Abdalah Kigoda na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mheshimiwa Mboni Mgaza.
 Wananchi wakifuatilia picha za matukio ya mkutano wa kuwashukuru wananchi.


 Mzee Yusuf akiwasalimu wakazi wa Tanga mjini ambapo anatazamiwa kutumbiza jioni ya leo kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa kama ahadi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyoitoa wakati wa ziara yake ya mkoa wa Tanga mwishoni mwa mwaka 2014.
 Wananchi wakiwa wamefurika uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi Desemba 2014.
 Umati wa watu
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akitoa salaam na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa Tangamano, Tanga mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye mkutano wa kuwashukuru wananchi walioichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 2014 nchi nzima ambapo mkoa wa Tanga umekuwa wa pili kwa kushinda kwa asilimia 97.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano ambapo alitoa salaam za mwaka huuambapo alisema CCM mwaka huu itaweka mkazo kwenye maadili ya Viongozi.
 Katibu Mkuu wa CCM akisisitiza jambo wakati wa kuwahutubia wananchi wa Tanga mjini
 Wananchi wakionekana kuhamasika na hotuba ya Kinana.


 Mnenguaji wa Jahazi Modern Taarab akiwapa mikono baadhi ya viongozi wakati wa kutoa bashraf kabla ya kuwatumbuiza wananchi jioni ya leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Mbaraka Saad Mbaraka akitangaza kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara mbale ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Tangamano.
 Hassan Omary Mbaraka aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia CHADEMA mwaka  2010 akitangaza kujiunga na CCM baada ya kumsikiliza kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Tangamano. Wananchi wa Tanga mjini wakimpa mkono wa kumuga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuwashukuru Watanzania kwa kuichagua CCM na kuwashukuru kwa imani yao kwa kutambua chama kinaweza kuongoza.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.