Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Neema Lugangira, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe CPA Amos Makalla amesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za tiba ya dharura ili kuongeza usalama wa wananchi, watalii, washiriki wa mikutano pamoja na kuifanya Arusha kuwa kitovu cha utalii wa kitabibu.
Akizungumza katika Mkutano wa Nane wa Afrika wa Tiba ya Dharura (AfCEM 2026) jijini Arusha, amesema Halmashauri sita za mkoa wa Arusha tayari zina idara za tiba ya dharura, huku Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na Hospitali ya Wilaya Karatu ina mitambo ya kuzalisha oksijeni. Aidha, amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu, vifaa tiba na upatikanaji wa huduma za kibingwa mkoani Arusha.
Ameeleza kuwa Serikali inajenga Hospitali ya Wilaya katikati ya Jiji la Arusha itakayokuwa na eneo maalumu la kutua helikopta (helipad), kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa wagonjwa wanaopata dharura katika hifadhi za taifa, maeneo ya utalii na kokote ndani ya mkoa wa Arusha.
Pia, amesema kuelekea kwenye AFCON 2027, mkoa wa Arusha umeweka kipaumbele katika kuongeza wataalamu wa afya na kuboresha huduma za tiba ya dharura ili kuhakikisha Arusha inakuwa tayari kutoa huduma za kitabibu kwa wananchi na wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇