Mwandishi mkongwe nchini, ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Uhuru la Kijani, Jane Mihanji amepokewa kwa shangwe kuu na Wafanyakazi wenzake wa UPL, alipowasili leo Ofisi za UPL akitokea mjini Dodoma, ambako alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Utafiti, Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia (RAAWU) kwa kipindi cha pili baada ya kupata kura 57 dhidi ya mpinzani wake, Benjamin Magori aliyepata kura 52.
Katika uchaguzi huo uliofanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa Saba wa Taifa wa RAAWU, kura 110 zilipigwa, huku mshindi akipatikana kwa tofauti ya kura tano.
Katika Ofisi za UPL Jane aliongozana na Katibu Mkuu Simon Mbay na Naibu Katibu Mkuu Kimoni Humbo.
Jane Mihanji akiingia ofizi za UPL kwa furaha
Baadhi ya Viongozi wa UPL wakiongozwa na Naibu Mhariri Mtendaji Madame Chacqueline Liana wakiwa tayari mumpokea Jane. Kisha akaanza kusalimana na wafanyakazi mbalimbali.
































No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇