Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Stanley Mkandawire (MNEC) ametoa rai kwa taasisi zinazoendelea na maandalizi ya michuano ya AFCON, Kama Tanesco, TARULA na DAWASA, kuhakikisha waandaa miundombinu mizuri ili kuipaisha nchi.
Ametoa mfano, kwa Tanesco kuhakikisha katika–katika ya umeme isiwepo kipindi chote cha Afcon, pia DAWASA nao wahikikishe wamejipanga vizuri, wawe na mpango mbadala kuhakikisha maji yatapatikana kipindi chote hata maji yakipungua mto Ruvu.
Katibu Mkandawire ametoa rai hiyo katika kikao cha Maandalizi ya michuano ya AFCON 2027, kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kabla ya rai hiyo, Katibu Mkandawire alimpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha viwanja vya michezo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo ya AFCON 2027.
Cde Mkandawire amesema kama Chama Wataendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kuhakikisha maandalizi haya yanakamilika kwa wakati na Tanzania inaendelea kulinda hadhi yake ya kimataifa.
Amesisitiza kila mwananchi kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazo tokana na mashindano hayo kwa kuwa yatafungua fursa za kiutalii na kibiashara.














No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇