Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Stanley Mkandawire (MNEC) jana, Novemba 12, 2026, alihudhuria Mkutano wa Sita wa Kimataifa kuhusu Ubora wa Elimu (IQEC), iliofunguliwa rasmi na Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ambao ni wa mwaka huu (2026) umebeba kaulimbiu inayolenga kujenga ustahimilivu wa kitaifa kupitia uhamasishaji wa rasilimali za ndani badala ya kutegemea misaada.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Waziri Mkuu alisisitiza mambo mbalimbali ikiwemo ufuatiliaji wa matokeo halisi shuleni na kuimarisha mapato ya ndani.
Katibu Mkandawire ameshiriki Mkutano huo ikiwa ni sehemu ya Chama kuendelea kuisimamia serikali kwa vitendo na kwa ukaribu juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika sekta ya Elimu
KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE








No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇