Mlezi wa CCM Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewataka viongozi na wanachama wa CCM kuzingatia Katiba, kanuni na taratibu za Chama katika kuelekea uchaguzi wa ndani wa mwaka 2027, akisisitiza kuwa nafasi za uongozi zinapaswa kupatikana kwa kuzingatia uwezo na sifa za mtu kuongoza badala ya kupanga safu kwa maslahi binafsi.
Chatanda ametoa kauli hiyo Novemba 7, 2026, katika ukumbi wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mara, alipozungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara, ambapo amekemea tabia ya baadhi ya wanachama kupanga safu za uongozi kabla ya uchaguzi na kuwataka kutoa haki na fursa sawa kwa wote wanaowania nafasi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇