ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assemblies of God Tanzania (KAG), Dkt. Evance Chande, amewataka Watanzania kukataa migawanyiko na kuwa makini dhidi ya watu wanaochochea mifarakano, akisisitiza kuwa kukubali hali hiyo kunaweza kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa nchi.
Akizungumza Novemba 8, 2026, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa la KAG, eneo la Lugala, Nala jijini Dodoma, Askofu Chande alisema wananchi wana wajibu wa kulinda umoja wa taifa kwa kutoruhusu tofauti mbalimbali kutumiwa kuwagawanya.
Alisisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kuwa sehemu ya kuimarisha mshikamano badala ya kuunga mkono vitendo vinavyoweza kuleta mifarakano katika jamii.
Kupitia harambee hiyo, jumla ya Sh milioni sita zilichangwa papo kwa papo, huku washiriki wengine wakitoa ahadi za kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha hatua hiyo ya ujenzi.
Ujenzi wa kanisa hilo kubwa umefikia hatua ya linta, hatua inayotangulia kuendelea na kazi nyingine za ujenzi kuelekea kukamilika kwa jengo hilo. KAG ina zaidi ya makanisa 50 nchini.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini kutoka madhehebu tofauti, waliotoka ndani ya Dodoma na mikoa mingine, ikiwa ni sehemu ya kushiriki tukio hilo la uwekaji wa jiwe la msingi.
Kwaya ya watoto ikitumbuiza.
Baadhi ya waumini na wageni waalikwa wakiwa katika sherehe hizo.


Askofu Mkuu Chande akihubiri.
Mchungaji wa kanisa hilo jipya, Mtema Chinyele akijitambulisha pamoja na mkewe Imelda.
Baadhi ya viongozi wa dini walioalikwa.









No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇