LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 8, 2026

UJUMBE WA MABUNGE DUNIANI (IPU) KUTOKA MATAIFA 16 WATEMBELEA MIRADI MIWILI YA MAENDELEO ARUMERU.


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Neema Lugangira amepokea ujumbe wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kutoka mataifa 16 ambapo wametembelea miradi miwili ya maendeleo ikiwemo mradi wa zahanati ya Kiyoga sambamba na mradi wa umwagiliaji wa vijana katika kijiji Cha Oloigeruno katika Halmashauri ya Arusha Dc.

Lugangira ameupongeza Ujumbe huo kwa kuendelea kuonyesha dhamira ya kushirikiana na serikali katika kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yenye mahitaji makubwa ya huduma za Afya na Kilimo.

"Sisi kama Arumeru tupo tayari kuendeleza ushirikiano huu na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini UNICEF, WHO, WFP pamoja na Mastercard Foundation na TAHA. Ombi langu kubwa ni miradi hii ifike maeneo mengine hapa Arusha DC na kwakuwa Wilaya yetu ina Halmashauri mbili ni muhimu sana tufike na Meru DC ili kuhakikisha tunachangia matokeo chanya na endelevu kwa wananchi wetu" amesema Lugangira . 

Kwa upande wake Hoyce Anderson Temu Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa ameeleza kuwa Tanzania imepata heshima kubwa kuwa mwenyeji wa Mkutano huu mkubwa na tunapaswa kujivunia.

"Mkutano huu ni mlango wa kufungua Mashirikiano na nchi mbalimbali duniani ,hivyo naendelea kusisitiza usimamizi mzuriii kwenye Miradi inayotekelezwa na Serikali na wadau wengine" amesema Temu

Lengo la zara hiyo ni Wajumbe hao kutembelea Wilaya ya Arumeru kujionea namna ambavyo huduma za afya ya Mama na Mtoto inavyotolewa kwenye Kituo Cha afya Kioga ,ambacho kilipata ufadhili na pia kujionea wa Vijana wa Umwagiliaji  na Mbogamboga.

Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani unaendelea jijini Arusha huku wageni kutoka mataifa mbalimbali wakiendelea kufurahia utajiri wa urithi na utamaduni uliopo nchini Tanzania.



DC Lugangira akizungumza na ujumbe huo.

Kilimo cha umwagiliaji.




 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages