LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 9, 2026

SPIKA WA AUSTRALIA DICK AUKWAA URAIS WA IPU

 Spika wa Baraza la Wawakilishi la Australia, Mhe. Milton Dick amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika Mkutano wa 153 wa IPU unaofanyika Arusha, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Uchaguzi huo umefanyika leo Oktoba 9, 2026 katika kikao kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Mhe. Dick ameshinda kwa asilimia 56  ya kura zote, huku akifuatiwa na Prof. Mhe. Sahiba Gafarova aliyepata asilimia 38 na Mhe. Robi Edwards amepata asilimia 6.

Mhe. Dick anachukua nafasi ya Dkt. Tulia Ackson wa Tanzania, ambaye anamaliza muhula wake wa miaka mitatu.

Mhe. Dick ni Mbunge wa Jimbo la Oxley, Queensland tangu mwaka 2016, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Spika mwaka 2022 na kuchaguliwa tena bila kupingwa mwaka 2025. 

Baada ya kuchaguliwa Mhe. Dick amesisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano kwenye umoja huo.

“Leo hakuna mshindi wala mshindwa. IPU imeongea kwa sauti moja. Hii ndiyo demokrasia. 

"Ni ukumbusho kuwa mazungumzo , heshima na ushirikiano bado vinaumuhimu. Tutafanya kazi pamoja, Tusikilizane, tutapata muafaka." amesema.

Mhe. Dick ataongoza mikutano ya kisheria ya IPU na kuiwakilisha taasisi hiyo katika matukio makubwa ya kimataifa, akifanya kazi kwa karibu na Katibu Mkuu Anda Filip.

Kuchaguliwa kwake kunaashiria sura mpya kwa IPU wakati wabunge wanaendelea kuimarisha majadiliano, uwakilishi wa kidemokrasia na ushirikiano wa kimataifa katika dunia inayokabiliwa na changamoto tata za kimataifa.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages