LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 15, 2026

MAJARIBIO YA KUONDOA VOCHA ZA KUKWANGUA KUANZA MWEZI UJAO KATIKA MIKOA MITANO

Kikomo cha kuanza kuondolewa kwa vocha za kukwangua nchini Tanzania kimepangwa kuwa Januari 1, 2027.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza hivi karibuni kuwa itaanza majaribio ya kusitisha matumizi ya kadi hizo za karatasi ili kuhamishia huduma zote kwenye mifumo ya kidijitali.

Mchakato huo utaanza kwa hatua zifuatazo:
Uhamasishaji kwa Umma: Ulianza rasmi tangu mwezi huu wa Oktoba 1, 2026, ili kuwandaa wananchi kisaikolojia na kiufundi.

Maeneo ya Majaribio (Kuanzia Jan 1, 2027): Majaribio yataanza katika mikoa mitano (5) mikuu hususan katika maeneo ya mijini yenye miundombinu wezeshi:

Dar es Salaam: Wilaya zote.

Dodoma: Jiji la Dodoma, Chamwino, Kondoa Mjini, na Kongwa.

Arusha: Jiji la Arusha, Wilaya ya Arusha, Meru, na Karatu.

Mwanza: Nyamagana, Ilemela, na Misungwi.

Mbeya: Jiji la Mbeya, Wilaya ya Mbeya, na Mbarali.

Mifumo Mbadala ya Kutumia:
Baada ya kikomo hicho, watumiaji katika maeneo yaliyotajwa watahitajika kuongeza salio au kununua vifurushi kwa njia za kidijitali pekee kama vile huduma za kifedha kwa mtandao wa simu (Mobile Money), rogramu za benki, au kupitia mawakala wa elektroniki.

Lengo kuu la Serikali na TCRA ni kupunguza utegemezi wa fedha taslimu, kuimarisha uchumi wa kidijitali, na kulinda mazingira dhidi ya taka za karatasi na plastiki zinazotokana na vocha za kukwangua.

Mbali ya lengo hilo la serikali, hatua hiyo ya kwenda kidijitali itaondoa adha ya kupoteza au Kukwangua vibaya vocha kabla ya kuitumia.


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages