LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 15, 2026

DC LUGANGIRA AWATEMBELEA VIONGOZI WA KIMILA WA JAMII ZA KIMAASAI NA WAMERU

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Neema Lugangira amefanya ziara ya kuwatembelea Viongozi wa Mila wa Jamii ya Kimaasai na Wameru kwa lengo la kujitambulisha, kuwaeleza juu ya mipango ya Serikali chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kufikisha maendeleo zaidi Arumeru, kuomba ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali. 

DC Lugangira amewapongeza na kuwashukuru Viongozi wa Kimila wa Jamii za Kimaasai na Wameru kwa kutambua umuhimu wa umoja, ushirikiano na amani na kuendelea kuitunza.  Amewasisitiza pia kuendelea kuheshimu,kulinda na kurithisha mila na desturi zao kwa kuzingatia maadili ya Taifa yanayoambatana na upendo,amani,utulivu na mshikamano nchini.

Kwa upande wao Viongozi hao wa Kimila, Laigwanani Mkuu Isack Ole Kisongo Meijo, Mwenyekiti Mkuu wa Viongozi wa Jamii ya Kimaasai nchini Tanzania na Laigwanani Amani Karaine Lukumay, Katibu Mkuu wa Viongozi wa Jamii ya Wamaasai nchini Tanzania pamoja na Mzee Wilson Mbise, Mshili Mkuu wa Jamii ya Wameru wamemshukuru Mkuu wa Wilaya Lugangira kwa kuwatembelea,unyenyekevu aliowaonyesha na wameaahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Arumeru inayounganisha Arusha DC na Meru DC huku wakiahidi kuendelea kuhubiri amani,upendo na mshikamano wa jamii katika maeneo yao na vikao vyao vya kimila. Wamemhakikisha watakuwa naye bega kwa bega na atafanya kazi zake kwa vizuri kabisa. 

Viongozi hao wa Kimila walimuombea na kumpa baraka zote Mkuu wa Wilaya Lugangira ili Mwenyezi Mungu aendelee kumpa baraka, hekima, maarifa na utashi zaidi katika kuwaletea wananchi wa Arumeru maendeleo.


 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages