LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 23, 2026

WAZIRI KAPINGA: HAKIKISHENI MNATUMIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA KWA UTOSHELEVU NA VIWANDA VYA NDANI ILI KULINDA SOKO

📌Azitaka taasisi za sekta binafsi na Masharikikisho ya wafanyabiashara kukumbushana misingi ya uendelevu wa Viwanda;


📌Awataka wafanyabiashara wazawa kuamini bidhaa zinazozalishwa na wazawa wenzao;


📌Mwekezaji kiwanda cha Simama Asema uwekezaji wa Bilioni 14 aliowekeza kuchechemua ari ya wazawa kwenye uwekezaji


Na Neema Chalila Mbuja

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga amevitaka Viwanda vinavyozalisha bidhaa kwa utoshelevu hapa nchini kuhakikisha vinalinda soko  la ndani na kuwataka wazawa kuamini bidhaa zinazozalishwa na wazawa wenzao


Mhe Kapinga ameyasema hayo Leo 23 Septemba, 2026 Jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizindua kiwanda cha kutengeneza vizibo cha Simama metal  crown kilichoko wilaya ya Kigamboni ambacho kinamilikiwa na mwekezaji mzawa kwa asilimia Mia moja.


Amezitaka taasisi za sekta binafsi Kama CTI, TPSF na TNBC kuhakikisha zinasimamia vema wamiliki wa viwanda na kuwakumbusha  misingi waliyojiwekea ya uendelevu wa viwanda.


Ameongeza kuwa bilioni 14 zilizowekezwa kwenye kiwanda hicho ni sehemu ya juhudi za kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje nakuongeza kuwa Serikali itaendelea kuhimiza umuhimu wa uwekezaji kwa wazawa na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara.


Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa Simama Tanzania Bwana Norbert Simama amesema kiwanda hicho cha vizibo kina uwezo wa kuzalisha visoda milioni 130 kwa mwezi kwa ajili ya matumizi ya viwanda vya vinywaji na kwa bora wa kimataifa na kumudu ushindani kimataifa..


Amesisitiza umuhimu wa viwanda vya vinywaji kushirikiana na kiwanda hicho kwa kutumia bidhaa zake, huku akibainisha kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini zinapaswa kuwa bora na kukidhi viwango vinavyohitajika ili kuongeza ushindani na kuimarisha soko la ndani.


Aidha, amesema mipango ya maendeleo ya viwanda inahitaji ushiriki wa sekta binafsi, huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji, akieleza kuwa kufikia uchumi wa dola trilioni moja kunategemea kwa kiasi kikubwa uwekezaji katika sekta ya viwanda.


Ametoa wito kwa wadau kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutimiza vigezo vya ubora ili kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za ndani na kukuza uchumi wa Taifa.























No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages