LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 1, 2026

MOI WAKO MGUU SAWA KUTOA HUDUMA MICHUANO YA AFCON 2027

 TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeanza kujiandaa kutoa huduma za kibingwa na kibobezi wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, zitakazoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.

Mkurugenzi Mtendani wa MOI, Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema taasisi hiyo imeweka mikakati ya kuimarisha wataalamu, vifaa tiba na mifumo ya huduma za dharura ili kuwa tayari kukabiliana na mahitaji ya kiafya yatakayojitokeza wakati wa mashindano hayo.

Dkt. Ulisubisya amesema MOI kwa sasa ina madaktari bingwa sita wa tiba za michezo ambao watakuwa sehemu muhimu ya utoaji wa huduma kwa wachezaji na watu wengine watakaohitaji matibabu yanayohusiana na majeraha ya michezo wakati wa AFCON 2027.

Amesema uwepo wa wataalamu hao sita haumaanishi kuwa MOI haina wataalamu wengine, bali madaktari hao wamebobea zaidi katika tiba za michezo, huku taasisi hiyo ikiwa na wataalamu wengine wa kutosha katika fani mbalimbali za tiba.

Hawa sita ni wataalamu waliobobea katika tiba za michezo, lakini si kwamba ndio wataalamu pekee tulio nao. Tuna wataalamu wengine wa kutosha ambao watahusika kulingana na mahitaji yatakayojitokeza,” amesema.

Kwa mujibu wa Dkt. Ulisubisya, maandalizi ya MOI yanaenda sambamba na kuimarisha mifumo ya dharura, upatikanaji wa vifaa tiba na uwezo wa wataalamu, pamoja na kujenga ushirikiano na taasisi nyingine za afya ili kuhakikisha wagonjwa wanaohitaji huduma za kibingwa wanapatiwa matibabu kwa wakati.

Amesema MOI iko tayari kushirikiana na Serikali, kamati za maandalizi ya AFCON pamoja na hospitali na taasisi nyingine za afya katika kuhakikisha huduma za afya zinakuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Tanzania katika kuandaa michuano hiyo.

Tumejiandaa kuhakikisha wakati wa AFCON 2027 tunakuwa sehemu ya kutoa huduma zinazohitajika. Tunaendelea kuimarisha wataalamu wetu, vifaa na mifumo ya huduma za dharura ili kukabiliana na mahitaji yatakayojitokeza,” amesema.

Dkt. Ulisubisya ameyasema hayo Septemba 1, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za MOI katika mwaka wa fedha 2025/2026 na mwelekeo wa taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

AFCON 2027 itakuwa ya kihistoria baada ya Tanzania, Kenya na Uganda kupewa jukumu la kuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa pamoja, huku maandalizi yakihusisha pia kuboreshwa kwa miundombinu ya viwanja, maeneo ya mazoezi, usafiri na huduma nyingine muhimu.

Kwa upande wake, MOI imeeleza kuwa itaendelea kujiimarisha ili kuhakikisha huduma za tiba za mifupa, ubongo na tiba za michezo zinapatikana kwa ufanisi wakati wa michuano hiyo.

Mkurugenzi Mtendani wa MOI, Dkt. Mpoki Ulisubisya,

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages