CCM Blog, Ilala
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi, amewataka vijana kuwa makini na ujumbe wanaoupoupata kutoka kwa baadhi ya viongozi kupitia mitandao ya kijamii, akisema wanapaswa kutafakari maslahi yao kabla ya kuchukua hatua kama za kushiriki katika maandamano.
Kihongosi amesema hayo leo Jumapili, Septemba 20, 2026, katika mkutano wa hadhara, akimzungumzia Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Mbunge wa zamani wa Tarime, John Heche, kuhusu ujumbe aliousema ameona umechapishwa na mwanasiasa huyo mtandaoni.
Amesema Heche amekuwa akiwahamasisha vijana na “masela” kushiriki maandamano, huku yeye akiwa anaendelea na shughuli zake za kilimo.
“Leo nimeingia mtandaoni nimeona Heche amepost kuwa analima maparachichi, hivi nchi ingekuwa haina amani angeweza kulima parachichi? halafu akija mtandaoni anawaambia vijana na ‘masela’ komaeni, andamaneni wakati huo yeye analima parachichi, akili za kuambiwa changanya na zako,” amesema Kihongosi.
Kihongosi amesema vijana wanapaswa kujiuliza kuhusu madhara na manufaa ya kushiriki katika shughuli zinazoweza kuvuruga utulivu, akisisitiza umuhimu wa kuelekeza nguvu zao katika shughuli za uzalishaji na kujenga uchumi wao.
Amesema maandamano yanayohamasisha vurugu hayana faida kwa vijana na kwamba familia za wanasiasa wanaotoa wito huo hazipaswi kuachwa kuwa mzigo wa vijana wanaoshiriki katika matukio hayo.
“Maandamano ya kweli ni kutafuta fedha na kutengeneza uchumi wako na wa familia yako,” amesema Kihongosi.





No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇