Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Asili hasa ya neno 'Hija' ambalo ni maarufu katika Kiswahili ni kutoka Kiarabu (Řج,) ambalo lina maana ya ziara au safari ya kwenda mahali maalum kwa lengo la kuwa karibu zaidi na ambako mambo muhimu ya historia yalitokea.
Awali lilimaanisha tu safari ya Waislamu kwenda Makka, kwa sababu katika utamaduni wa Waswahili neno hili lilikuwa kama ni kufanya safari ya kidini pekee.
Baadaye Wakristo nao walilipokea neno hili na kulitumia kutaja safari zao za kiroho na sasa siku hizi neno hili Hija kwa jumla linatumiwa na dini zote kutaja safari za aina hii.
Baadhi ya dhini kama Wahindu huhiji mahali pengi hasa mji wa Benares na mto Ganges, Uyahudi nako kulikuwa na hija ya kwenda Yerusalemu, iliyokuwa ya lazima katika sikukuu mbalimbali kwa waumini kuanzia umri wa kubalehe; iliendelea hata baada ya hekalu la mji huo kubomolewa kabisa mwaka 70 BK.
Wakristo hasa wa Kiorthodoksi na Katoliki wanajua hija ya kwenda Yerusalemu, Roma na mahali pengine huku Waislam huwa na hija ya kwenda Makka, Washia wanatembela pia makaburi ya maimamu wao huko Najaf, Karbala, Mashhad na penginepo. Mwislamu aliyetimiza safari hii anapokea cheo cha "alhaji" kama sehemu ya jina lake.
Kwa uchache hiyo ndiyo maana ya neno 'Hija', na nimekuandikia utangulizi huo, kusudi nikueleze kwamba sasa kuna Hija ambayo inaitwa 'Hija Halisi' ambayo yenyewe hufanyika mkoani Kigoma.
Hija hii, hufanywa kila mwaka na Kanisa Halisi la Muumba, ambao hufika kuhiji kwa sababu wanapafahamu kuwa kuwa hapo Kigoma, ndiyo Bustani Halisi, (bila shaka kwa wale wanaojua maana ya Bustani kutoka maandiko watakuwa wanajua ina maana gani Kigoma kuitwa hivyo).
Kanisa Halisi la Muumba, Kao lake Kuu ni Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam. Lipo chini ya Mwenyekiti anayetambulika kwa jina la BABA HALISI ambalo ni jina kama jina, siyo cheo kwa sababu kwenye Kanisa hilo hakuna hadhi ya Cheo, hii ikiea ni kwa kuwa Kanisa lina uelewa kuwa Cheo kina kikomo lakini Safu ina mwendelezo.
Kwenye Safu hiyo kuna MAMA HALISI ambaye ni Mwenza wa BABA HALISI, MNARA MMOJA HALISI, UDHIHIRISHO HALISI, WATEKELEZA SAUTI HALISI na UZAO HALISI ambao ni waleo waliompokea BABA HALISI au katika jamii huitwa wafuasi.
WATEKELEZA SAUTI ni Wasimamizi wa Vituo vya Kanisa Halisi vya ngazi za Kao Kuu, Mikoa, Wilaya na hata kwenye Vitongoji na katika Jamiii.
Kwa nini Hija Halisi Kigoma?
Kuhusu Hija hii kufanyika Kigoma, BABA HALISI anafafanua kwamba ni kutokana mkoa huo sasa kuwa ndiyo Bustani Halisi, kutokana na kwamba yeye alipata uheri wa kupokea Sauti Kuu ya Muumba wa Wote, Yote na Vyote mara nne (2015, 2019, 2020 na 2023) akiwa Kigoma.
BABA HALISI anazitaja Sauti hizo kuwa ni; Sauti Mpya ambayo imetangaza kuwa Tanzania ni Taifa Baba, Sauti Mpya ambayo imetangaza kuwa Afrika ni Bara la Nuru, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya zile Sauti Saba, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya ishara tatu mbinguni (Ufunuo 12:1-9) na Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya Nafsi ya Moyo (Miungu tisa mitakatifu iliyofafanuliwa ndani ya Kitabu ambacho katika jamii huitwa Biblia.
"Kigoma, Tanzania na Afrika tujitambue kuwa tuna Sauti Mpya ambayo inabadilisha maisha mabaya kuwa mazuri, Sauti Mpya imebeba kila kitu kizuri.
Hija hii ya Chanzo Halisi (MUUMBA) inayofanyika Kigoma, siyo maigizo wala usanii, ni halisi", anasema BABA HALISI akifafanua umuhimu wa Hija hiyo na kwa nini inabidi ifanyike Kigoma kila mwaka na kuongeza kuwa Sauti hiyo mpya sasa imepokelewa katika mabara yote kwa utukufu wa MUUMBA.
Anaweka wazi kwamba Sauti hiyo Kuu iyopokewa sio ya kidini wala ya kidhehebu au ya Huduma binafsi, kama baadhi wanavyoweza kudhani, bali ni kwa faida ya wote, bila kujali dini, dhehebu au mtu yeyote.
"Katika matendo 8:27-39, tunashuhudia jinsi watu mashuhuri na wasio mashuhuri, walivyokuwa wakienda Mashariki ya Kati kuabudu, wengine walienda kwa magari, ndege na wengine kwa meli.
Tulichokuwa tunafuata kule Mashariki ya Kati ni Sauti iliyosikika kule. Sasa Sauti ya Uhai iko Tanzania. Watu wote Kaskazini, Kusini. Mashariki na Magharibi mwa Uumbaji wote wajue kuwa Hija ya CHANZO HALISI iko Tanzania, mjini Kigoma. Kama walivyokuwa wakiendesha magari, ndege na meli kwenda mashariki ya kati sasa waje Tanzania", anasema BABA HALISI.
Anasema, imethibitika kuwa Hija Halisi iko Kigoma Tanzania, baada ya kuwa wamefanya Ibada ya Hija kuanzia Mwaka 2018, 2019, 2020, 2021, 2023 na kuendelea bila tatizo lolote na kwamba uthibitisho wa Dk. Livingstone, Waarabu, Wajerumani na Wamisionari wa Kiswidishi ambao waliweka Ngome Kigoma -Ujiji bila kusema sababu kwa wakati ule ni dhahiri kwamba kumbe walikuwa wanasaka Sauti ya CHANZO HALISI ambayo walijua itatokea Kigoma (Ingawa walifichwa Majira sahihi).
Sasa katika mwendelezo wa Hija hiyo Halisi, tayari Kanisa Halisi limeshafanya maandalizi makubwa ya Hija ya kumi (10) kwa mwaka huu (2026), safari na Kuwasili Kigoma imepangwa Kuanza Tarehe 1-3 Oktoba 2026
ambalo Mahujaji (Uzao) wataanza safari kuelekea mkoani Kigoma kwa njia mbalimbali za usafiri zilizoratibiwa na Dawati la Hija
Wageni na Uzao wote watapokelewa na kuwekwa kwenye kambi na maeneo maalum yaliyoandaliwa karibu na Bustani Halisi (eneo la Chanzo cha Sauti) mkoani Kigoma.
Kilele cha Ibada ya Hija kitafanyika Tarehe 4 Oktoba 2026 / 26 Thebeti 1Majira Halisi, kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 11:00 jioni.
Msikilize BABA HALISI, akieleza kwa NINI Hija Kigoma?👇

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇