Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis F. Mdaku, ameshiriki mafunzo ya kimataifa yanayolenga kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji, uhifadhi wa udongo na mabwawa, yanayofanyika nchini China.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Wizara ya Biashara, yakiwakutanisha viongozi na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali kujifunza mbinu za kisasa za kudhibiti mafuriko, mmomonyoko wa udongo na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza wakati wa ushiriki mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Mdaku alisema maarifa anayoyapata yatachangia kuimarisha juhudi za Tanzania katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji na maendeleo ya jamii.
"China imeonesha namna ambavyo teknolojia, mipango madhubuti na usimamizi wa kisayansi vinaweza kulinda vyanzo vya maji na kupunguza athari za mafuriko. Uzoefu huu ni muhimu kwa Tanzania, hususan katika kuimarisha usalama wa maji kwa wananchi,” amesema Dkt. Mdaku.
Ameongeza kuwa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya maji unafungua fursa ya kubadilishana uzoefu na kutumia mbinu bora zinazoweza kuboresha huduma za maji na kuhifadhi mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇