Benki ya NMB imetunukiwa cheti cha hadhi ya Superbrand Afrika Mashariki kwa kipindi cha 2026–2028 baada ya kupata kura nyingi zaidi za watumiaji katika kundi la benki, kwa mujibu wa Baraza la Superbrands.
Utambuzi huo umetokana na tathmini iliyohusisha Baraza la Superbrands na watumiaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni ubora wa bidhaa na huduma, utofauti wa chapa pamoja na uwezo wa kutoa huduma kwa kiwango kinachofanana kwa muda.
Mjumbe wa Baraza la Superbrands, Dorine Bangapi, alisema hadhi hiyo haiwezi kununuliwa, kwa kuwa uteuzi hutokana na maoni na kura za watumiaji. Alisema NMB ilipata kura nyingi zaidi katika kundi la benki.
Cheti hicho kilipokelewa kwa niaba ya NMB na Mkuu wa Idara ya Masoko, Rahma Mwapachu. Benki hiyo imesema utambuzi huo unaongeza wajibu wa kuendelea kuboresha huduma na kulinda imani ya wateja wake.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇