Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) haijaridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Mzumbe kuhusu hoja zilizobainishwa katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Devotha Minja, amesema Kamati imebaini dosari katika matumizi ya fedha za umma, ikiwemo manunuzi yaliyofanyika bila kuzingatia matakwa ya Sheria ya Manunuzi ya Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Agosti 18, 2026, Bungeni jijini Dodoma, Mheshimiwa Minja amesema PAC haijaridhishwa na majibu ya Chuo kuhusu hoja hizo na kwamba baadhi ya maelezo yaliyotolewa hayajatoa majibu ya kuridhisha kwa Kamati.
Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG, Chuo hicho kilifanya manunuzi yenye thamani ya Sh bilioni 29.77 kutoka kwa wazabuni ambao hawakukidhi vigezo, huku Sh bilioni 1.54 zikilipwa kwa watu ambao hawakukidhi viwango vilivyowekwa.
Aidha, Kamati imeeleza kutoridhishwa na ujenzi wa barabara yenye thamani ya Sh milioni 523, ambayo imeelezwa kuwa ilijengwa chini ya kiwango kilichotakiwa.
Hoja nyingine iliyozua wasiwasi ni madai ya malipo ya ziada yenye thamani ya Sh milioni 718, ambayo kwa mujibu wa Kamati hayakustahili kulipwa na hayakuzingatia masharti yaliyokuwa kwenye mkataba.
Mheshimiwa Minja amesema kutokana na uzito wa hoja hizo, Kamati inaendelea kutafakari hatua zaidi za kuchukua ili kutoa ushauri unaostahili kwa Bunge.
Kamati ya PAC ilikuwa ikijadili Taarifa ya Hesabu Zilizokaguliwa za Chuo Kikuu cha Mzumbe pamoja na hoja zilizoibuliwa na CAG katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2024/2025.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Devotha Minja (kushoto) akiongozi kikao cha kamati hiyo wakati wa kujadili Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Chuo Kikuu cha Mzumbe pamoja na hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2024/2025, jijini Dodoma Agosti 18, 2026.Kulia kabisa ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aesh Hilaly.
Vikao vya kamati za Bunge vinaendeleo kwenye kumbi mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge la 13 unaotarajiwa kuanza Jumatano Agosti 26, 2026.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Devotha Minja (kushoto) akiongozi kikao cha kamati hiyo wakati wa kujadili Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Chuo Kikuu cha Mzumbe pamoja na hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2024/2025, jijini Dodoma Agosti 18, 2026.Kulia kabisa ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aesh Hilaly.
Vikao vya kamati za Bunge vinaendeleo kwenye kumbi mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge la 13 unaotarajiwa kuanza Jumatano Agosti 26, 2026'
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Aesh Hilaly (kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Moris Makoi.
Wajumbe wa kamati hiyo ya PAC wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakijitambulisha katika kikao hicho.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA.- 0754264203
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇