LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 11, 2026

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KUPITIA TUZO ZA MONDE SELECTION

 

 Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeendelea kuthibitisha ubora wa bidhaa zake katika jukwaa la kimataifa baada ya kutunukiwa Gold Quality Awards kutoka taasisi ya kimataifa ya Monde Selection, kupitia bidhaa zake za Serengeti Lite, Serengeti Lager, Serengeti Lemon pamoja na TZee.

Tuzo hizi zinatolewa kwa bidhaa zinazokidhi viwango vya juu vya ubora duniani baada ya kufanyiwa tathmini ya kina na jopo huru la wataalamu wa kimataifa. Bidhaa hupimwa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo ubora wa bidhaa, ladha, mwonekano, ubunifu, taarifa kwa watumiaji pamoja na uzoefu wa matumizi, kwa lengo la kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa vya ubora.

Monde Selection ni taasisi ya kimataifa ya kutathmini ubora wa bidhaa za walaji iliyoanzishwa mwaka 1961 jijini Brussels, Belgium. Kwa zaidi ya miaka 65, taasisi hiyo imekuwa ikifanya tathmini za kitaalamu kwa maelfu ya bidhaa katika makundi mbalimbali ikiwemo vyakula, bia, vinywaji, vileo, bidhaa za afya na lishe pamoja na vipodozi. Tathmini hizo hufanywa na zaidi ya wataalamu 80 wa kimataifa, huku bidhaa kutoka takribani nchi 150 zikiwa zimewahi kufanyiwa tathmini na kutambuliwa kwa ubora wake.

Mafanikio haya yanaendelea kudhihirisha dhamira ya SBL ya kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kiwango cha dunia kupitia uwekezaji endelevu katika teknolojia za uzalishaji, mifumo madhubuti ya udhibiti wa ubora na ubunifu unaoweka mahitaji ya watumiaji mbele.

Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Ugavi wa SBL  Joseph Cheloti, alisema ushindi huo ni uthibitisho wa juhudi za kampuni katika kuhakikisha kila bidhaa inayowafikia watumiaji inazingatia viwango vya juu vya ubora.

"Kupokea Gold Quality Awards kutoka Monde Selection ni heshima kubwa kwetu na uthibitisho kuwa bidhaa zetu zinakidhi viwango vinavyotambulika kimataifa. Tunajivunia mafanikio haya ambayo yanatokana na kujitolea kwa wafanyakazi wetu, ubora wa malighafi tunazotumia pamoja na mifumo yetu ya uzalishaji. Zaidi ya yote, tunawashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuamini na kutuchagua kila siku."

Aliongeza kuwa kampuni itaendelea kuwekeza katika ubora, ubunifu na maendeleo ya bidhaa zake ili kuhakikisha Watanzania na watumiaji katika masoko mengine wanaendelea kupata bidhaa zenye viwango bora vinavyotambulika duniani.

Kutunukiwa kwa bidhaa nne kwa wakati mmoja kunaiweka Serengeti Breweries Limited miongoni mwa wazalishaji wanaoendelea kuonesha ushindani katika sekta ya vinywaji kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyotambulika kimataifa, huku ikiendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania katika soko la dunia.

Kuhusu Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ni moja ya kampuni zinazoongoza katika sekta ya vinywaji nchini Tanzania na ni sehemu ya Diageo PLC, kampuni inayoongoza duniani katika biashara ya vinywaji. Kampuni inazalisha na kusambaza bidhaa mbalimbali zinazopendwa na Watanzania ikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Serengeti Lemon, Pilsner Lager, Guinness, Senator, Kibo Gold, Smirnoff Ice, Johnnie Walker, Bailey's pamoja na TZee.

SBL inaendelea kuwekeza katika ubora wa bidhaa, maendeleo ya jamii, uhifadhi wa mazingira, kilimo endelevu na ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia shughuli zake za biashara na ushirikiano na wadau mbalimbali.

 

Kuhusu Monde Selection

Monde Selection ni taasisi huru ya kimataifa inayobobea katika kutathmini ubora wa bidhaa za walaji, iliyoanzishwa mwaka 1961 jijini Brussels, Belgium. Kwa zaidi ya miongo sita, taasisi hiyo imekuwa ikitambua bidhaa zinazokidhi viwango vya juu vya ubora kupitia World Quality Awards, zinazotolewa baada ya tathmini ya kina inayofanywa na jopo la wataalamu wa kimataifa.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, zaidi ya bidhaa 9,000 kutoka duniani kote zimefanyiwa tathmini na majopo ya Monde Selection. Kila mwaka, zaidi ya wataalamu 80 kutoka fani mbalimbali, wakiwemo wataalamu wa ladha, ubora wa bidhaa, lishe, kemia, uhandisi wa chakula na afya, hushiriki katika mchakato wa kupima na kutathmini bidhaa kwa kutumia viwango vya kisayansi na kitaalamu.

Tuzo za Gold Quality Award hutolewa kwa bidhaa zinazofikia viwango vya juu vya ubora baada ya kupitia mchakato huo wa tathmini. Leo, alama ya Monde Selection inatambulika duniani kama ishara ya ubora, uaminifu na uthibitisho wa viwango vya kimataifa vya bidhaa.


 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages