Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Halima Okash amekutana na viongozi wa CPCT Wilaya ya Chemba waliomtembelea ofisini kwa lengo la kumjulisha kuhusu ujio wa wageni kutoka taasisi ya World Hope International watakaotekeleza mradi wa uchimbaji wa visima vya maji katika shule za msingi zote wilayani humo.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mkuu wa Wilaya alisema hatua hiyo ni muhimu katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wanafunzi pamoja na kuimarisha mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.
Alieleza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, CPCT na World Hope International unaonesha dhamira ya pamoja ya kuboresha huduma za jamii, hususan sekta ya elimu, kupitia miradi yenye manufaa ya muda mrefu.
Mkuu huyo wa Wilaya aliishukuru World Hope International kwa moyo wake wa kujitolea na kuwakaribisha rasmi wilayani Chemba, akieleza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi na kuwanufaisha wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla.
#JeshiLaMamaKazini


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇