Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku, inawapongeza vijana wote wa Bendi ya Muziki ya Malinyi waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kozi ya muziki na sanaa.
Tunawataka wanufaika wote waliotajwa kufika kwa wakati katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Victory siku ya Jumamosi, tarehe 01 Agosti 2026, ili kuanza rasmi mafunzo yaliyodhaminiwa na Mheshimiwa Mbunge.
Hii ni hatua muhimu ya kuwawezesha vijana kukuza vipaji vyao, kujenga taaluma, na kufungua fursa mpya katika sekta ya sanaa na muziki.
Hongereni kwa wote mliochaguliwa. Tunawatakia mafanikio mema katika safari yenu ya kujifunza na kutimiza ndoto zenu.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇