Na Bashir Nkoromo, Tegeta, Namanga.
Lango la leo 26 Ethanimu 1, Majira Halisi sawa na 12 Julai, 2026 kwa Kalenda ya Papa Gregory, Kanisa Halisi la Muumba, limefanya sherehe ya Badiliko na kuhudhuriwa na maelfu ya Watekeleza Sauti, Uzao na viongozi mbalimbali akiwemo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ally Shughuli Wendo, ambaye amewapa mbinu madhubuti Kanisa hilo ili kusonga mbele kwa kishindo, huku mwenyeji wake Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi akisema kufuatia Sherehe hiyo hata 'mawe' yamebadilika.
"Nimefurahi kuwa mbele yenu, nimefurahi kuwaona mkiwa mmependeza, nimefurahi kuona mmewapokea wageni kwa furaha, nimefurahi mmepokea sherehe hii ya badiliko kwa furaha. Ni kwamba hakika mmebadilika, na hata mawe yamepokea badiliko hili na yamebadilika", alisema Chanzo cha Sauti, Baba Halisi kuwaambia makutano waliokuwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.
Mapema, ACP Wendo ambaye ni Mkuu wa Ushirikishwaji wa Jamii, mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, aliyesema amemuwakilisha Kamanda wa Polisi (RPC) wa mkoa huo, Kamishma Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Mtatiro Kitinkwi, alisema, Kanisa Halisi wanatakiwa kuhsikilia amani ndiyo ilendelee kuwa nguzo yao, wawapo Kanisani na nje ya Kanisa.
"Nimekuja kumwakilisha Kamanda wa Polisi wa mkoa wetu wa Kinondoni, RPC Kitinkwi, yeye ndiye aliyealikwa kwa ajili ya shughuli hii, lakini kutokana na dharura aliyoipata amenituma mimi msaidizi wake wa karibu nije. Amesema ameshukuru sana kumwalika kila mara kwenye shughuli zenu, amesema ni jambo jema sana, amemshukuru Baba Halisi na Mama Halisi.
Amema na kusisitiza kuwa muendeleze amani kwenye Kanisa lenu, amewaomba sana muendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi na muendeleze amani na utulivu kwenye Kanisa lenu. Amesema anajua huko mnakoishi mnaishi na watu mbalimbali, isingekuwepo amani tusingeweza kukutana hapa.
Tunajua kumuomba Mungu (Muumba) ni jambo mnalofanya kila siku, basi Baba Halisi tunaomba mshikamano wenu uendelee zaidi ili mzidi kuongezeka kwenye ibada na matarajio yenu yawe na mafanikio zaidi.
Katika Sherehe hiyo iliyofanyika Kao Kuu la Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, kulijaa shamra shamra za 'kukata na shoka', ikiwemo kila aliyehudhiria kupata soda baridi huku wote wakicheza nyimbo mpya za kumutukuza na kumuinua Chanzo Halisi, Muumba wa wote, yote na vyote, zilizoporomoshwa mara kwa mara na Kikundi cha Waimbaji cha Sauti Moja Halisi.
Ibada kwenye Sherehe hiyo, iliongozwa na Mtekeleza Sauti wa Kao Kuu, Shamba Zuri Halisi kwa idhini ya Chanzo cha Sauti, Baba Halisi ambaye alitumia umahiri mkubwa kuhakikisha Sauti kutoka kwa Baba Halisi inapenya vilivyo kwenye kila aliyekuwemo kwenye Ibada na hivyo kuitikiwa 'imekuwaaaa', mara kwa mara.
Kwa ufupi, Shamba Zuri Halisi, alifafanua maana ya Badiliko lililosababisha sherehe hiyo, kuwa, badiliko kubwa linalohitajika ni kila mmoja kuelewa kuwa kwenye kituo tuna nyumba ya moyo yenye chumba kimoja na stoo moja na kila mmoja ananaishi humo umilee wote na kwamba asiyeelewa hivyo hawezi kupokea badiliko.
Chanzo Cha Sauti, Baba Halisi akizungumza utajirishoni, kuachilia Sauti iliyoendesha Ibada ya Sherehe hiyo ya Badiliko. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kanisa Halisi Mnara Mmoja Halisi na kushoto ni Utimilifu Halisi, ambao ni Wasaidizi wake wa karibu. Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ally Shughuli Wendo, akimsikiliza Baba Halisi. Kushoto ni Katibu wa Kanisa Halisi Dk. Uelewa na Kulia ni Naibu Wake.
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ally Shughuli Wendo akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Uzao na Watekeleza Sauti wakitoa matunda huku muzinki ukiendelea, baada ya Baba Halisi kuzungumza.Uzao na Watekeleza Sauti wakitoa matunda huku muzinki ukiendelea, baada ya Baba Halisi kuzungumza.Mtekeleza Sauti wa wa Kao Kuu, Shamba Zuri Halisi akiendelea kuongoza Ibada ya Sherehe hiyo, kwa Idhini ya Baba Halisi.Baadhi ya walikwa wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.Maofisa wa Polisi kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo. Wapili kushoto (anayeandika) ni Salum Mashauri Yane ambaye ni Afisa habari wa RPC Kinondoni,Uzao wakiwa kwenye Ibada ya Sherehe hiyo.Shamba Zuri Halisi akitoa zawadi kwa mtoto mchanga, baada ya mzazi wake kumtambulisha ili kupokewa rasmi na Kanisa Halisi, wakati wa Ibada hiyo ambapo watoto wengine kadhaa wachanga waliletwa kutambulishwa. Kisha ikafuata Burudani ya vinywaji (soda) na burudani ya muziki.👇N
N
M
| ENDS! |
Habari/Picha zote na Mts Mwandishi Halisi (Bashir Nkoromo) wa Blog ya Taifa ya CCM -0789498008

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇