LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 20, 2026

MIKOPO YA NMB YA MIFUGO YAVUKA SH.BIL. 180

Benki ya NMB imetoa zaidi ya Sh180 bilioni kufadhili wafugaji na biashara katika mnyororo wa thamani wa mifugo, ikiwemo unenepeshaji, uzalishaji wa malisho, ununuzi wa mbegu bora na ujenzi wa miundombinu ya kisasa.


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema hayo katika ufunguzi wa Tri-Nations Livestock Expo 2026 uliofanywa na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, katika viwanja vya Mbogo Ranches, Ubena Zomozi, Chalinze. NMB ni mdhamini mkuu kwa mwaka wa nne mfululizo.

Mponzi alisema mikopo hiyo inatolewa kwa riba nafuu ya asilimia tisa, huku mkakati wa NMB wa agribusiness na agri-wholesale ukilenga kufadhili wafugaji, wazalishaji wa malisho, wanunuzi, wasindikaji na biashara kubwa katika sekta hiyo.

Dk. Nchemba aliwataka wafugaji kutumia elimu na teknolojia inayopatikana katika maonesho hayo kukabiliana na uhaba wa malisho na kuongeza tija.

NMB imesema itaendelea kutoa elimu ya fedha, ushauri wa biashara, mikopo na bima kupitia matawi 248, mawakala zaidi ya 75,000 na huduma za kidijitali ili kusogeza huduma karibu zaidi na wafugaji nchini.

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, kuhusu mikopo, elimu ya fedha na huduma za kibenki kwa wafugaji alipotembelea banda la NMB katika Tri-Nations Livestock Expo 2026, Mbogo Ranches, Ubena Zomozi wilayani Chalinze, mkoani Pwani. 



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages