LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2026

TUTAANZISHA MFUKO WA MAFUTA- KIHONGOSI

 

SERIKALI imeamua kuanzisha Mfuko Maalumu utakaosaidia kupunguza makali ya bei ya mafuta ambayo imepanda kufuatia vita vinavyoendelea kati Israel, Marekani na Irani.

Mpango huo umeelezwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Makao Makao ya CCM.jijini Dodoma Aprili 7, 2026.

Amesema kuwa CCM na Serikali itahakikisha mafuta yanapatikana wakati wote na kwa bei nafuu.

Aidha, Kihongosi amesema kuwa  Serikali pia ina mpango wa kutoa ruzuku katika mafuta kama ilivyofanya wakati wa vita vya Urusi na Ukraine ambapo Serikali ilitoa  bil. 100.



 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0715264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages