LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 19, 2026

MAMBO YA MBUNGE MWALUNENGE BUNGENI DODOMA WIKI HII

 

Mwalunenge akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima walipokutana kwenye viunga vya Bunge Dodoma, baada ya kushiriki mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Katikati ni Mbunge wa Morogoro Kusini, Zubery Mfaume.

Mbunge wa Mbeya Mjini, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wakuu wa mikoa waliohudhuria kikao cha wabunge kujadili makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni Dodoma mwanzoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi  Macha na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.


Akioneshwa jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule walipokuwa wakitoa bungeni wakati wa mapumziko.

Mwalunenga (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa mikoa.

Patrick Mwalunenge akiiomba serikali kuuruhusu mkoa huo kukopa fedha za kujenga Km 100 za Jiji la Mbeya na kwamba uwezo wa kulipa deni hilo wanao. bungeni Dodoma Aprili 14, 2026. Pia Mwalunenge ameiomba serikali kuupatia mkoa huo fedha zitakazosaidia kukarabati masoko mbalimbali ya Jiji hilo ambayo yamechakaa. Ameyasema hayo alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu.

Mwalunenge akiwa kwenye viwanja vya Bunge Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages