Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ambaye pia ni mratibu wa kitaifa wa mpango wa kuzuia na kupambana na majanga ya kikemia, kibaolojia, kira diolojia na kinyuklia (CBRN) Prof. Najat Kassim Mohammed wakati wa kikao kati ya wawakilishi kutoka Jumuiya ya Ulaya na wajumbe wa kitaifa wa mpango wa kukabiliana na majanga ya kikemikali, kibaolojia, kiradiolojia na kinyuklia.
Prof.
Najat ameongeza kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ili kuongeza
uelewa wa wanachi na wadau mbalimbali wa kemikali, hasa katika
kuwajengea uwezo katika kukabiliana na hatari zinazotokana na sumu za
mabaki ya kemikali sambamba na kusaidia watendaji wa mipakanai
kudhibiti uingizwaji wa kemikali zenye sumu nchini sambamba na kujenga
utamaduni wa kutumia kemikali kwa matumizi salama.
Kwa
upande wake kiongozi wa utekelezaji wa mradi namba 111 katika kuzuia na
kupambana na majanga na madhara ya mabaki ya kemikali kupitia harakati
za Jumuiya ya Ulaya (EU CBRN CoE) Bw. Pablo Taboada ametoa taarifa ya
mradi huo kwa wajumbe wa kitaifa wa mpango wa kukabiliana na majanga ya
kikemikali, kibaolojia, kiradiolojia na kinyuklia.
Wajumbe
wa Timu ya Taifa ya CBRN pamoja na wawakilishi wa mamlaka na za
serikali na wadau wa kemikali wamekutana kujadili kwa kina fursa ambazo
Tanzania inaweza kuzipata kupitia mradi huo. Katika kufafanua. Pablo
amesema mradi huo wa Umoja wa Ulaya una lengo la kusaidia nchi za Ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati katika kupambana na hatari (sumu)
zitokanazo na matumizi/mabaki ya kemikali ndani ya jamii.
Katika
taarifa hiyo. Pablo ameongeza kuwa mradi huo namba (EU P111)
umelenga nchi 11 ambazo ni Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Ethiopia, Kenya, Ghana, Zambia, Uganda, Seychelles, Rwana na
Malawi ambapo pamoja na taasisi zinazosimamia usalama kwa wananchi
kujengewa uwezo mradi huo utaenda sambamba na kutoa mafunzo kwa shule za
sekondari na vyuo vya kati na vyuo vikuu ili kuwajengea wanafunzi uwezo
wa kutambua madhara ya sumu za kemikali ili waweze kujua na kujikinga,
na kutoa elimu hiyo kwa jamii.
Kwa
upande wake Meneja wa usajili wa kemikali na maabara za kemia Mamlaka
ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bwn. Musa Kuzumila amesema mradi
huo utawasaidia katika utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali
yanayohusika na usimamizi na udhibiti wa utumiaji wa kemikali hapa
nchini.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇