Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi (Mb), umefikishwa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli ya kuaga inayotarajiwa kufanyika kesho tarehe 28 Machi, 2026 katika Viwanja vya Karimjee.
Mwili huo umesafirishwa leo tarehe 27 Machi, 2026 baada ya shughuli ya kuaga iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Mhe. Lukuvi amefariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.





No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇