LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 8, 2026

TUZO YA HESHIMA KUTOKA KWA WANAWAKE WA UBUNGO


Katika kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, nimeguswa sana kupokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa wanawake wenzangu wa Ubungo. Tuzo hii si yangu pekee, bali ni ishara ya juhudi za pamoja tunazozifanya katika kuimarisha nafasi ya mwanamke katika jamii na uchumi wa nchi yetu.

Nilipata heshima ya kipekee ya kufungua Kongamano la 'Wanawake Nguvu ya Jamii' lililoandaliwa na UWT Wilaya ya Ubungo katika Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC), Ubungo Machi 06, 2026.

Nawashukuru sana UWT Wilaya ya Ubungo kwa maandalizi haya na kwa heshima hii kubwa. Tuendelee kuwa nguvu ya mabadiliko! 

#MwanamkeNguvuYaJamii
 #SikuYaWanawakeDuniani2026 
#MaendeleoYaWanawake





 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages