LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 7, 2026

DKT MAJULE KUPELEKA MSAADA WA VITI BAISKELI 25 KWA WATU WENYE ULEMAVU

Mbunge wa Viti Maalumu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Neema Majule katika kuunga mkono tabasamu la Rais Samia Suluhu Hassan kwa Watu wenye ulemavu ameamua kutoa msaada wa viti baiskeli 25 kwa watoto 12 na wanawake 13 mkoani Dodoma. Akizungumza hivi karibuni baada ya kutoa msaada mwingine wa vyakula, vinywaji na vifaa vya usafi kwa Shule ya Viziwi Dodoma, Dkt. Majule ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Rhema Education Foundation aliahidi kutoa msaada huo wa vifaa hivyo saidizi kwa Watu wenye ulemavu, kwa nia ya kupeleka tabasamu, heshima na matumaini mapya kwa Watu wenye ulemavu pamoja na kuwatia moyo na kuimarisha Wanawake wanaolea watoto hao wenye ulemavu. Hafla hiyo ya kukabidhi vifaa hivyo, inatarajiwa kufanyika Machi 8, 2026 majira ya saa 8 mchana katika Kata ya Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203
 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages